Chama Cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) leo Aprili 5, kwa kushirikiana na Hospitali ya Narayani India wametoa elimu ya afya pamoja na ushauri wa kitaalamu kwa wanahabari wanawake kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya afya ya uzazi na magonjwa na magonjwa ya saratani.
Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa TAMWA, Bi. Alakok Mayombo alisema washiriki wa mafunzo hayo watajengewa uwezo kuhusu afya ya uzazi pamoja na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.
“Katika kipindi cha siku mbili za mkutano mkuu wa chama chetu, Tulizungumza na marafiki wa TAMWA Narayana hospital ambao walikubali kutoa elimu ya afya uzazi kwa wakina mama kupitia kipengele chao cha awareness kuhusu hasa magonjwa ya kansa" Alisema Bi. Mayombo.
Alisema kupitia elimu ambayo itatolewa kwa washiriki hao itawawezesha kuwasaidia kujilinda na kupambana kansa kwa akina mama.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Rose Reuben, alisema, mbali na mafunzo hayo ya afya ya uzazi pia watatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya ya mitandao ya kijamii.
“Ni lazima jamii itambue sheria ya maudhui ya mtandao pamoja na sheria za vyombo vya habari katika mitandao ya kijamii. Lengo letu ni kujiongezea ujuzi katika maeneo haya, hivyo watu wa TCRA watakuja kutusaidia kutoa mafunzo kuhusu matumizi ya mtandao ni”. Alisema Rose.
Nae daktari kutoka Hospitali ya Narayana, Bwana Limbanga Freddie alisema, tafiti zinaonyesha kumekuwepo na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kansa kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha pamoja na kutofanya mazoezi, kutokufanya kazi ngumu na kutumia vyakula ambavyo ni hatari kwa afya.