Press Release

MIAKA 37 YA TAMWA, 30 YA BEIJING, UKATILI KWA NJIA YA MTANDAO, TISHIO JIPYA

User Rating: 4 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Inactive
 

Novemba 25, 2024.Dar es Salaam.Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinaungana na watanzania, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali na watanzania kwa ujumla katika kuadhimisha Siku 16 za Ukatili wa Kijinsia.

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zina adhma ya kukumbusha jamii kuhusu mienendo na mitazamo inayochagiza vipigo, ukeketaji, ubakaji, ulawiti, mimba za utotoni na rushwa ya ngono katika jamii. 

Kadhalika,siku hizi 16 zinatumika kutafakari kwa Pamojani wapi tulipofanikiwa, wapi penye mapengo nnikwa namna gani tutayaziba mapengo yaliyopo katika kupunguza ukatili wa kijinsia. 

Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu ni: Kuelekea miaka 30+ ya Beijing: Tuungane kumaliza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto

Kauli mbiu hii inalenga kuwakumbusha viongozi, wanaharakati na wadau wa masuala ya ukatili wa kijinsia hasa serikali, sekta binafsi na kampuni kuchukua hatua ili kumaliza ukatili huu.

Kama dhima ya mkutano wa Beijing, ilivyokuwa, kadhalika TAMWA kwa miaka 37 sasa kimebeba ajenda ya kumaliza ukatili wa kijinsia katika Nyanjazote, nakatika msimu huu bado kinaikumbusha jamii kuondokana na dhana potofu zote zinazomdunishakumnyima fursa , kumuharibia utu na kumwondolea staha, na wakati mwingine kusababisha ulemavu nhatakifo mwanamke na mtoto wa kike

Dhana hizo ni Pamojana mwanamke hawezi kuwa kiongozi, mtoto wa kike hana haja ya kupata elimu, ukeketaji, ubakaji na ulawiti.

Katika miaka 37 ya kufanya kazi katika eneo hili, tumeona mafanikioambayo kwa kushirikiana na serikali, tumeweza kupiga hatua na sauti zikasikika kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii,” Dr Rose Reuben, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA.

Tumefanikiwa kupata sheria ya makosa ya kujamiiana ya SOSPA na tumefanikisha kuingizwa kwa kipengele cha rushwa ya ngono katika sheria ya rushwa. 

“Haya ni mafanikio ambayo tunajivunia katika miaka hii 37 ya uwepo wa TAMWA” Dr Rose

Hata hivyo bado kuna changamoto zinazoibuka ambazo zinachagizwa na kukua kwa teknolojia, sisi tumeona ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kijinsia kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Matumizi ya mitandao ya kijamii licha ya kuwa yameleta maendeleo lakini wanawake wamekuwa wakiathiriwa na mitandao hiyo kwa picha zao kusambazwa, au picha mjongezinazowadhalilisha zikisambazwa.

“Tumepata kesi kadhaa za Watotowa kike kutishiwa kutoa kiasi cha fedha kwa sababu wenza wao waliwarekodi picha za utuputunapokea kesi ambapo wanawake wanabakwa na kisha kupigwa picha zinazosambazwa mitandaoni,” Dr Rose 

Pamoja na hayo, kadhalika tumeona wanawake wanasiasa wakidhalilishwa mitandaoni hali inayochagiza kuacha kushiriki katika siasa au kuacha kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye jamii.

Hivyo basi TAMWA, katika kipindi hiki cha Siku 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia, tunakemea udhalilishaji wa wanawake kwa kutumia mitandao ya kijamii

Tunawahimiza wanawake na Watotowa kike,wasiogope kutoa taarifa kwa mamlaka husika ikiwamo TAMWA, ambayo chini ya kitengo cha Usuluhisi wa Migogoro, (CRC) imekuwa ikisaidia wanawake/Watotowa kike wanaokumbana na udhalilishaji wa ain azote.

CRC itasikiliza kesi yako kwa hali ya faragha na kutoa msaada wa kisheria ili mwathirika apate haki yake” Dk Rose Reuben. 

TAMWA inatathmini miaka yake 37 ya harakati za kumaliza ukatili wa kijinsia katika mifumo yote na hata sasa inaendelea kuihimiza jamii kutathminimiaka 30 ya mkutano wa Beijing, kwa kuangazia nafasi ya wanawake wanasiasa, wanahabari na wanawake wote ambao wamekuwa walengwa katika ukatili wa kijinsia kwa njia ya mtandao. 

Kwa kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ina neno ‘Kuungana’ hivyo basi TAMWA tunahimiza  tuungane, wanaofanya ukatili huo wachukuliwe hatua bila kujali nafasi zao, ikiwezekana mikakati ya kitaifa ifanyike kuwasaidia wanawake na Watotowa kike wanaodhalilishwa mitandaoni

TAMWA inawaita wanawake na Watotowa kike wanaokumbana na ukatili mtandaoni na ukatili mwingine wowote, kuwasiliana kwa namba:  au kufika ofisi za TAMWA, Sinza, Mori kuanzia leo Novemba 25 hadi Desemba 10, kupata msaada wa kisheria bure. 

Mkurugenzi Mtendaji

DkRose Reuben

TAMWA

Search