- TAMWA
- Hits: 422
Female Genital Mutilation | Ukeketaji



Chama cha Wanahabari Wanawake –TAMWA, kinaungana na mashirika mengine yanayopinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu kote nchini kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 16 Juni kila mwaka.
Maadhimisho hayo ambayo yatafanyika wilayani Ilala Kata ya kivule leo tarehe 14 Juni, 2018 kuanzia saa tatu Asubuhi hadi saa tano katika viwanja vya stendi ya Mbondole, Mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Sophia Mjema ambapo kauli mbiu mwaka huu ni “Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tusimwache Mtoto Nyuma’’ inamlenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa, jirani na rafiki kumpenda mtoto kwa namna yoyote ile, kuhakikisha anatunzwa vizuri na haki zake zinalindwa ipasavyo ili atimize ndoto zake.
Zaidi ya Wanachama 150 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA, Jumamosi tarehe 14th April, 2018 wanafanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2017 ambapo pamoja na mambo mengine, wanachama watapata fursa ya kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2017, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2018-2019.
Chama cha Wanahabari Wanawake - TAMWA kimefurahishwa na kinazidi kuupongeza Umoja wa Wabunge Wanawake nchini kwa juhudi ambazo unaendelea kuonyesha kutafuta kiasi cha Sh.3.2bilioni za kujenga vyoo vya mfano kwa wanafunzi wasichana na wenye mahitaji maalumu katika majimbo 264 ya uchaguzi nchini.