- TAMWA
- Hits: 564
Right for education | Haki ya elimu




Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinaungana na taasisi nyingine nchini kulaani vikali matukio ya mauaji ya wanawake na watoto yaliyotokea hivi karibuni hapa nchini.
Kwa kadri siku zinavyoendelea mauaji ya wanawake na watoto yanayotokana na sababu mbalimbali yameripotiwa kutokea sehemu mbalimbali hasa katika maeneo ya Njombe, Rombo, Mto wa Mbu na Simiyu.
Pamoja na matukio ya mauaji ya watoto Njombe na Simiyu, hivi karibuni kumetokea mauaji ya wanawake Arusha na mikoa mingine.
TAMWA tunasikitishwa na mauaji hayo na tunaikumbusha jamii kuwa kila mtu anayo haki ya kuishi kulingana na sheria na taratibu za nchi yetu.
Hivyo tukiwa wadau wanaosimamia haki za wanawake na watoto tunakemea haya na kuwataka wadau wengine kuanzia ngazi ya familia hadi serikalini kuwalinda watoto na kuhakikisha kuwa migogoro ya kifamilia inamalizwa kwa mazungumzo ya amani.
Tumeona na tunapongeza juhudi kubwa zilizofanywa na vyombo vya usalama nchini lakini pamoja na juhudi hizo cha kujiuliza ni kuwa kwanini bado matukio haya ya mauaji yameendelea kuripotiwasiku baada ya siku?
Tunachelea kwamba, matukio haya yasipoundiwa mifumo ya muda mrefu ili kuyakomesha kabisa, basi tutaendelea kupoteza kinamama na watoto ambao kimsingi ni nguvu kazi ya Taifa.
TAMWA tunapendekeza uwepo wa mfumo endelevu utakaohusisha wadau mbalimbali wakiwemo wananchi, vyombo vya usalama na kampuni za simu kuwezesha waathirika kutoa taarifa za dalili zozote za ukatili kabla haujatokea.
TAMWA tunaungana na familia za waathirika wa matukio haya tukiwatakia faraja katika kipindi hiki kigumu.
Rose Reuben
Mkurugenzi Mtendaji
TAMWA
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA leo, kinaungana na mashirika yote nchini yanayotetea haki za binadamu hasa wanawake na watoto ulimwenguni kusherekea siku ya wanawake duniani ambayo huadhimishwa tarehe 8 mwezi Machi kila mwaka.
Maadhimisho haya yanabeba kauli mbiu ya kitaifa inayosema “Wakati ni sasa: Wanaharakati Mijini na Vijijini kubadilisha maisha ya wanawake”, ambayo inatutaka wote tushirikiane kikamilifu kubadilisha maisha ya wanawake kwa kuondokana na ukatili wa kijinsia ili kupanua wigo wa fursa za usawa kiuchumi kwa wanawake.
Tarehe 16 Julai, 2018,Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia idadi ya watu duniani (UNFPA),lina Ujumbe Kutoka Jumuia ya Umoja Ulaya (EU) kwa Tanzania Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), Ubalozi wa Uingereza, Ubalozi wa Ireland, Ubalozi wa Uholanzi, pamoja na ubalozi wa Kanada kwa pamoja watakuwa wenyeji wa shughuli ya kuonesha juhudi zinazohitajika katika kukomesha suala la ukeketaji hapa nchini. Katika tukio hilo Kutakuwa na hotuba kutoka kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na Watoto. Pia kutakuwa na Hotuba ya mwakilishi wa Jeshi la polisi Tanzania na wanaharakati wa haki za binaadamu pia kutakuwa na uzinduzi wa filamu mpya yenye hadi ya kimataifa inayoitwa “In the Name of Your Daughter”,. Baadsa ya filamu hiyo kutakuwa na wasaa wa maswali na majibu kutoka kwa washiriki wa tukio hilo.
Dk. Kaanaeli Kaale ameanza rasmi safari ya kuongoza Bodi ya TAMWA kwa miaka mitatu baada ya kuchaguliwa na wanachama wa TAMWA katika Mkutano Mkuu uliofanyika jijini Dsm tarehe 28 June 2025 .
Dk. Kaale ameahidi kuendeleza mafanikio ya waliotangulia na kuhimiza matumizi ya TEHAMA, usawa wa kijinsia na uandishi wa haki kipindi hiki cha uchaguzi.
#TAMWAAGM2025 #TAMWA #WanawakeViongozi #UsawaWaKijinsia #HabariNaTEHAMA
Baada ya miaka 6 ya mafanikio makubwa, Joyce Shebe anamaliza muda wake kama Mwenyekiti wa bodi ya TAMWA.
Amewaachia wanachama kumbukumbu ya #TuzozaSamia Kalamu, maadhimisho ya miaka 36 ya TAMWA, na uwekezaji imara wa taasisi.
Asante kwa uongozi uliotukuka!
#TAMWAAGM #TAMWA #JoyceShebe #WanawakeViongozi #MafanikioYaUongozi #TuzoZaSamiaKalamu