Gallery

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Dar es Salaam, Septemba 10, 2025.Chama cha WanahabariWanawake Tanzania (TAMWA) kinatoapongezizadhatikwawanawakewotewaliojitokezakuwanianafasizauongozikuanziangaziyaudiwaniubungehadiuraiskatikamchakatowa uchaguzimkuu wa Oktoba 29, 2025.

Mchakatowauteuzinauchukuajifomuumeonyeshaarinamwamkomkubwa wa wanawakekushirikikwenyenafasimbalimbalizauongozinchiniKwamujibuwatakwimuzaUlingoWanawakejumlayawanawake 231 walichukuafomuzaubungekupitia CCM, nakatiyao 25 waliteuliwanachamananewakiwaniwapyaAidhamwakahuuvyamavingivyasiasavimeongezaidadiyawanawakewagombeawenzakatikanafasiyauraisnamakamu wa Rais.

Kwanamnayakipekee, TAMWA inampapongezizapekeeMheshimiwaSamiaSuluhu Hassan, aliyeteuliwana CCM kuwamgombea wa kwanza mwanamke wa uraiskatikahistoriayachamatawala.Hiinihatuakubwanayakihistoriainayoashiriamapinduzinamwelekeompya wa ushiriki wa wanawakekatikauongozi wa juunchini

PiatunawatambuawanawakewenginewalioteuliwakugombeauraispamojanawagombeawenzaakiwamoMwajumaNotyMiramboaliyechukuafomuyakuwaniauraiskupitia Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD), akiwanamgombeamwenzaMashavuAlawiHaji.Wagombeawenza w niEvelineWilbardMunis- NCCR, Husna Mohamed Abdallah-CUF, Aziza Haji Selemani-MAKINI, Amani Selemani Mzee-TLP, ChausikuKhatibu Mohamed-NLD, Sakia Mussa Debwa-SAU,  ChumaJumaAbdallahnaDevothaMinja- CHAUMA. 

TAMWA inatambuanakuthaminiujasirinakujitumakwawanawakewotewaliojitokeza au kujaribukugombeanafasihizilichayachangamotombalimbalizinazowakabili.

Kwamudamrefu, TAMWA imekuwamstariwambelekuhamasishaushiriki wa wanawakekatikasiasanauongozikupitiawarshamakongamanomijadalanavyombovyahabariilikuondoavikwazovinavyowakabiliwanawakeMafanikiohayanihatuamuhimukuelekealengo la kuonawanawakewakiongozakatikangazizamaamuzinakuchocheausawa wa kijinsia.

RipotiyaOfisiya Taifa yaTakwimu (NBS) inaoneshakuwahadiFebruari 2024, wanawakewalikuwaasilimia 37.4 yawabunge (148 katiya 392), wengiwaowakiwakupitiavitimaalum.RipotizaAprilinaJulai 2024 zinaonyeshaasilimia37.5 yamawaziriniwanawake.

Lichayamafanikiohayabadojamiiinakabiliwanachangamotozinazotokanana  mfumodumenaudhalilishaji wa wanawakehasakwenyemitandaoyakijamii. TAMWA inaendeleakutoaelimukupitiavyombovyahabarikuhakikishawanawakewanasiasawanashirikikampenikatikamazingirarafikiyenyeusawanausalamakamailivyo wa wagombeawanaumebilakubaguliwakwamisingiyajinsia.

Uwepowawanawakekwenyeuongozinimuhimukwamaendeleoyataifakwanihuletausawa wa kijinsiakatikajamiiuwajibikajinakulindamaslahiyamakundiyotehususanwanawakenawatotoKukosekanakwawanawakekatikanafasizajuukunadhoofishautekelezaji wa sheriana sera zakulindahakizawanawakenawatotoikiwemokupambananaukatili wa kijinsiandoanamimbazautotoniukeketajinaudhalilishaji wa kijinsianamakundiyawatuwenyemahitajimaalum.

TAMWA inasisitizaniwajibu wa jamiivyamavyasiasaserikalinawadau wa maendeleokuhakikishawanawakewanapatanafasisawakwenyesiasanauongoziilikujengataifalenyeusawa wa kijinsiaamaninamaendeleoendelevu.

Kadhalikatunatoawitowakampenisafinajumuishizenyestahazinazolengakujengaustawinautu wa jamiibadalayasiasazamatusinakejeliTamwainafuatilia  kampenikatikangazizotenahaitasitakuripotimgombeayeyote au kundiambalolitakiuka  kanunizauchaguziilisheriaichukuemkondowake.

Dkt. Rose Reuben

Mkurugenzi  Mtendaji.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania - TAMWA, Jumamosi 14/04/2018 kimefanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2017 ambapo pamoja na mambo mengine,  wanachama walipata fursa ya kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2017, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2018 - 2019. Mkutano huo ni wa 30 tangu kuanzishwa chma hicho na ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.

 

Mwenyekiti wa TAMWA Bi Alakok Mayombo, akizungumza jambo wakati wa mkutano

 

Mwanzilishi wa TAMWA Bi Fatma Alloo, akizungumza na wanachama wakati wa mkutano mkuu

 

Baadhi ya Wanachama wa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

February 19,2014

 

Board Member of the Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) Gladness Hemed Munuo launching a Gender Based Violence survey report which was conducted in December 2013 in 20 districts of Tanzania Mainland and Zanzibar today at the association’s office in Sinza Mori, Dar es Salaam.

The Tanzania Media Women’s Association (TAMWA) today February 19,2014, released a Gender Based Violence survey report which was conducted last year in twenty districts of Mainland Tanzania and Zanzibar. The report was unveiled to journalist by the association’s board member Gladness Hemedi Munuo today at Sinza – Mori.

The survey is a result of training conducted with the support from UNFPA in which 30 journalists from across the country were sent to the regions to conduct survey.

The report highlights the real situation of GBV in the surveyed areas and factors limiting stakeholders’ efforts to defending women and children rights in the country.

In Tanzania Mainland, the survey was carried out in the following districts and respective regions in brackets; Kahama (Shinyanga), Tarime (Mara), Sengerema (Mwanza), Newala (Mtwara), Mbulu (Manyara), Singida Rural (Singida), Bariadi (Simiyu), Busega (Simiyu), Nkasi (Rukwa), Dodoma (Dodoma), Babati (Manyara), Chunya (Mbeya) and Bunda (Mara) while in Zanzibar, the survey was conducted in six districts from regions of Mjini Magharibi, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Unguja Kusini and Kaskazini Unguja.

 

For information  Download the report in English version here and Swahili version here

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

 Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kimefadhaishwa na kinalaani vikali vitendo vya mauaji vinavyoendelea kutekelezwa na baadhi ya wanandoa kwa makusudi na kuwanyima haki ya kuishi wenza wao kwa kuwaua  kinyama kwa sababu ya wivu wa mapenzi. 

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

TAMKO LA ASASI ZA WANAWAKE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Dar –Es- Salaam, Oktoba 23, 2025.
Wakati Watanzania wakielekea katika tukio la kikatiba la kupiga kura mnamo Oktoba 29, muunganiko wa asasi za kiraia zinazotetea makundi maalum ikiwamo wanawake, watoto na vijana wanawake, tumeungana kwa pamoja kuhimiza umma kuhusu ajenda muhimu ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi sambamba na kuhimiza ushiriki wa wanawake katika upigaji kura siku ya Oktoba 29 mwaka huu.

Ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi ni miongoni mwa vipaumbele vya asasi za kiraia zenye mrengo wa jinsia. Kwa sababu tunaamini wakiwapo viongozi wanawake, kutakuwa na hatua mahsusi katika kuongeza kipato na maendeleo ya mwanamke.

Hivyo basi sisi muunganiko wa asasi za kiraia, tunawahakikishia kuwa tunakwenda kutimiza wajibu wetu wa kikatiba wa kupiga kura na kadhalika tunahimiza wanawake kwenda kushiriki katika mchakato wa kikatiba wa kupiga kura, ili tunapokwenda kuwachagua viongozi wetu, basi tuwatwike mzigo wa mambo ya msingi yanayowahusu wanawake .

Viongozi hawa tutakaowachagua, tunaamini kuwa baada ya mchakato huo, tutawatwika madai yetu ya kimaendeleo yanayowahusu wanawake, watoto, wanawake vijana na watu wenye ulemavu na ajenda nyinginezo za mrengo wa jinsia.

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimepiga hatua katika ajenda ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi. Kwa mara ya kwanza Tanzania imepata kiongozi mkuu wa nchi mwanamke, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye pia anawania kiti hicho cha urais kwa tiketi ya CCM.

Kadhalika, mwaka huu kumekuwa na wagombea wengine wanawake wa urais, akiwemo Saumu Rashid kutoka UDP na Mwajuma Mirambo –UMD.

Kwa upande wa wagombea wenza wa urais kutoka vyama vingine ni pamoja na Eveline Wilbard Munis (NCCR), Husna Mohamed Abdallah (CUF), Aziza Haji Selemani (D. MAKINI), Amani Selemani Mzee (TLP), Chausiku Khatibu Mohamed (NLD), Sakia Mussa Debwa (SAU), Chuma Juma Abdallah na Devotha Minja (CHAUMA).

Hii ni hatua kubwa ya kidemokrasia kwa Tanzania na kwa ajenda ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi.

Tunapokaribia uchaguzi mkuu, tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa mwanamke kiongozi anaposhika madaraka asihukumiwe kwa jinsia yake, bali kwa uwezo, uzoefu na dira yake ya maendeleo.

Ikumbukwe kuwa uongozi wa mwanamke si tishio bali ni nyenzo ya kuimarisha demokrasia jumuishi, yenye kusikiliza na kutenda kwa manufaa ya wote.

Tunapenda kuikumbusha jamii kuwa katika kipindi hiki cha kampeni na uchaguzi, ni muhimu kuepuka lugha za kejeli, udhalilishaji na mashambulizi ya kibinafsi — hasa kwa misingi ya kijinsia. Badala yake, mjadala wa kisiasa ujikite katika sera, ilani, na hoja zenye kujenga taifa.

Wanawake wanaowania nafasi kuanzia ngazi ya udiwani hadi urais, wasibezwe, wasitukanwe, na tunakemea vikali lugha dhalili zinazotweza utu kwa wanawake wanasiasa na viongozi wengine wanawake.

Bado tunaamini kuwa kwa kumpata Rais mwanamke Tanzania imepiga hatua kubwa kupitia yeye katika kutekeleza Dira ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDG 5) inayosisitiza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika maamuzi.

Kupitia Rais huyu mwanamke tumeona sheria kadhaa zikibadilishwa ikiwamo ya vyama vya siasa na hata miradi mikubwa ya maendeleo ikiwamo ya afya.

Asasi za kiraia zinasimama imara katika kuhakikisha kuwa mafanikio haya yanaendelezwa, si kwa maneno tu bali kwa vitendo.

Ushiriki wa wanawake katika siasa unaongeza uwajibikaji, uwazi, na ustawi wa kijamii, kwa kuwa tafiti nyingi zinaonesha kwamba wanawake viongozi wanapendelea sera zinazogusa elimu, afya, haki za watoto, na usawa wa kiuchumi. Kama zipo changamoto kupitia uongozi wake basi si muda wa kumkashifu kwa kupitia jinsia yake.

Tunapenda pia kuikumbusha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), vyama vya siasa, na wadau wote kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa salama, jumuishi, na huru dhidi ya vitisho, udhalilishaji, na ukatili wa kijinsia, ambao mara nyingi huwakatisha tamaa wanawake kushiriki kikamilifu katika siasa.

Tunatoa wito kwa vyombo vya habari kuendelea kutoa nafasi sawa kwa wagombea wanawake kuratibu midahalo, makala, na mijadala inayojenga uelewa wa umma juu ya uwezo na mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa.

Kwa muktadha huu, tunasema: “Uongozi bora hauna jinsia — una maadili, dira, na dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.”

Tunaamini kuwa taifa lenye usawa wa kijinsia katika uongozi ni taifa lenye amani, ustawi, na maendeleo endelevu.Tanzania ni yetu sote — wanawake na wanaume wanapaswa kushiriki kwa usawa katika kuijenga.

Imetolewa na:
Muunganiko wa Asasi za Wanawake na Watetezi wa Usawa wa Kijinsia – Tanzania

(Oktoba 23, 2025 – Dar es Salaam)

  1. Ulingo Wanawake

  2. Women Walfare Tanzania

  3. TAMWA

  4. Binti Makini-

  5. WAJIKI-

  6. WILDAF-

  7. WFT-

  8. Young and Alive

  9. Generation Act

  10. TAWIA

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

CHAMA CHA WANAHABARI WANAWAKE TANZANIA TAMWA  kinawatangazia  wanachama  wake  kuwa  kutakuwa  na  Mkutano  Mkuu  wa  Wanachama (AGM)   utakaofanyika  Juni 13-14, 2025.

LENGO LA MKUTANO MKUU WA AGM NI:

• Uchaguzi wa wanachama  wapya  kwamujibu   wa Katiba ya Chama.
• Tathmini ya  mwenendowa chama – mafanikio, changamoto, namwelekeompya.
• Uwasilishajiwa  taarifa  ya  mapato  namatumizi  ya chama.
• Uwasilishaji  wa  taarifa za   utekelezaji  wamiradi  namustakabali  wa TAMWA.
• Fursaya   wanachamakutoa  maoni  namapendekezo  ya  kuimarisha  mchangowa TAMWA katikajamii.

Mkutano huu utafanyika tarehe 13-14 Juni, 2025

• Eneo: Ukumbi wa TAMWA, Sinza, Mori, Dar es Salaam
• Moduli: Kwa kufika ofisi za TAMWA na kwa njia ya Zoom 
• Muda: Saa 4 asubuhi

Wanachama  wote  mnahimizwa  kuhudhuria

Kwa maelezo  zaidi, tafadhaliwasiliananaTAMWA kupitia;

Barua pepeThis email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Simu:0716622200

Search