Chama cha Wanahabari Wanawake –TAMWA, kinaungana na mashirika mengine yanayopinga ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu kote nchini kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo huadhimishwa tarehe 16 Juni kila mwaka.
Maadhimisho hayo ambayo yatafanyika wilayani Ilala Kata ya kivule leo tarehe 14 Juni, 2018 kuanzia saa tatu Asubuhi hadi saa tano katika viwanja vya stendi ya Mbondole, Mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Sophia Mjema ambapo kauli mbiu mwaka huu ni “Kuelekea Uchumi wa Viwanda, Tusimwache Mtoto Nyuma’’ inamlenga kila mzazi, mlezi, ndugu, jamaa, jirani na rafiki kumpenda mtoto kwa namna yoyote ile, kuhakikisha anatunzwa vizuri na haki zake zinalindwa ipasavyo ili atimize ndoto zake.



