- TAMWA
- Hits: 1516
TAMWA YAMCHAGUA MWENYEKITI MPYA WA BODI
Aprili 6, 2019. Wanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA), kimemchagua Joyce Shebe kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi ya chama hicho.
Aprili 6, 2019. Wanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA), kimemchagua Joyce Shebe kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi ya chama hicho.

Godwin Assenga, Tamwa.
Dar es Salaam. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) kinatoa pongezi za dhati kwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu na Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebecca Gyumi kwa kushinda tuzo ya Umoja wa Mataifa katika kipengele cha utetezi wa haki za binadamu kwa mwaka 2018.
Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Maria Fernanda alimtangaza Gyumi pamoja na washindi wengine, Octoba 25 mwaka huu.
Washindi wengine ni marehemu Asma Jahangir , mwanasheria wa Haki za Binadamu wa Pakistan, Joenia Wapichana, mwanaharakati wa haki za watu wa jamii za pembezoni wa Brazil na taasisi ya Front Line Defenders, inayojihusisha na ulinzi wa haki za binadamu, Ireland.
“TAMWA inaamini kuwa, ushindi wa Gyumi ni ushindi kwa watoto na wanawake wote nchini ambao haki zao zimekuwa zikikandamizwa,” anasema Edda Sanga, Mkurugenzi, TAMWA.
Wengine waliowahi kushinda tuzo hii miaka ya nyuma ni pamoja na aliyewahi kuwa mke wa Rais wa Marekani, Franklin Roosevelt, Eleanor Roosevelt, mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa dini wa Marekani, Martin Luther King.
Wengine ni aliyewahi kuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu(ICRC)
Sherehe za utoaji wa tuzo hizi zitafanyika Desemba huko New York, Marekani.

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania,(TAMWA), tumepokea kwa masikitiko kifo cha mmiliki wa kampuni za IPP nchini, Dk Reginald Mengi ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT.
Kifo hiki ni pigo kubwa kwa tasnia ya habari nchini, pia kwa jamii ya Watanzania hasa kwa watu wenye ulemavu.
Dk Mengi ameacha alama katika tasnia ya habari kwa kuanzisha vyombo vya habari na alibeba dhamana ya kuwa mlezi kwa wanahabari nchini, na alileta heshima katika tasnia hii nchini.
Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tuzo za umahiri wa habari za Ejat hasa katika maudhui kuhusu watu wenye ulemavu, ambako amekuwa akidhamini tuzo hizo.
Atakumbukwa kwa upendo wake mkubwa kwa wenye ulemavu. Dk Mengi amekuwa muumini mzuri wa masuala ya usawa wa kijisia katika taasisi zake ambapo ametoa nafasi za ajira na za uongozi kwa wanawake na wanaume.
Pia Dk Mengi alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini.
Dk Mengi alikuwa na ndoto nyingi, mojawapo ni ya kushirikiana na serikali kutokomeza umaskini kama alivyoandika kwenye ukurasa wake wa twitter Machi 19, ''Ndoto yangu ni kushirikiana na serikali kutokomeza kabisa umaskini Tanzania''
Ulale salama Dk Mengi, tutaendelea kuyaishi maneno yako kwa mfano nukuu yake ya Januari 7 aliyotuma kupitia mtandao wake wa twitter akisema: ''Kwa unyenyekevu ninawashauri watanzania wenzangu kuufanya mwaka 2019 kuwa mwaka wa upatanisho na msamaha, chuki ni mzigo mzito kuubeba mioyoni mwetu, kupendana ni njia peee ya kusonga mbele''.
Pumzika kwa amani Dk Mengi.
Rose Reuben
MKurugenzi TAMWA
Godwin Assenga, Tamwa
Kisarawe. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeadhimisha Siku ya mtoto wa kike Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe.
Maadhisho hayo yalifanyika kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na wadau wa masuala ya jinsia.
Siku ya mtoto wa kike huadhimishwa Oktoba 11 kila mwaka ambapo mwaka huu maadhikisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo; “Imarisha uwezo wa mtoto wa kike” Tokomeza Ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kazimzumbwe iliyopo Wilaya ya Kisarawe na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe, Mussa Gama.
Katika maadhimisho hayo watoto walipata fursa ya kufikisha ujumbe wao mbele ya mgeni rasmi kwa njia mbalimbali ikiwamo maigizo, ngonjera na risala.
Pia TAMWA kwa kushirikiana na kampuni ya Asas Diary waligawa maziwa kwa wanafunzi walioshiriki maadhimisho hayo.
Wanafunzi toka shule mbalimbali wilayani Kisarawe wakifanya maandamano
Mmoja wa wanafunzi akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa
Kikundi cha skauti kisarawe wakionyesha gwaride mbele ya mgeni rasmi
Kikundi cha maigizo kisarawe kikifanya igizo la madhara ya ukeketaji mbele ya mgeni rasmi