Gallery

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
  1. Tuliweza kufanya mahojiano na Mwanaharakati, Waziri na Balozi wa zamani, Mama Getrude Mongela: Finya hapa kupata zaidi: https://www.instagram.com/p/C4DCBDJNGr4/
  1. Tuliweza kufanya mahojiano na Mkurugenzi wa TAMWA, Dk Rose Reuben: Finya hapa kusikiliza zaidi: https://www.instagram.com/p/C4M_5NHtZO3/
  1. Tuliweza kufanya mahoajino na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Ana Makakala: Kusikiliza zaidi. Finya hapa: https://www.instagram.com/p/C5IOVDJNSnh/
  1. Tuliweza kufanya mahoajino na Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Doroth Semu: Kusikiliza zaidi finya hapa: https://www.instagram.com/p/C4qSGabtrrZ/
  1. Tulikuwa na Makala fupi ya video ya Dereva wa Bodaboda Singida, Marry Kalambwa” Finya hapa kumfahamu: https://www.instagram.com/p/C4ulIZvNZpF/
  1. Tulikuwa na Makala fupi ya video ya Semeni Kalori: Semeni: Mama wa watoto watano, anayeendesha bodaboda, kusomba mkaa milimani. Finya hapa kumjua zaidi: https://www.instagram.com/p/C4hyRrmtevi/
  1. Tulikuwa na Makala fupi ya video ya Paulina Mathayo, anayeponda kokoto, huko Dodoma; Finya hapa kumfahamu: https://www.instagram.com/p/C5ILJSSthYu/

Tembelea mitandao yetu:

       1.Twitter: https://twitter.com/TAMWA_ 

  1. Instagram: https://www.instagram.com/tamwa_/
  2. Facebook: https://www.facebook.com/media.womenassociation

       4. TAMWA TV: //www.youtube.com/@tamwaonlinetv7655 

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Sekretarieti ya Chama cha Wanahabri Wanawake Tanzania – TAMWA, inapenda kuwakumbusha wanachama wake kuwa mkutano mkuu wa Chama kwa mwaka 2022, utahusisha uchaguzi wa wajumbe wa Bodi, hivyo tunawahimiza wanachama wanaowiwa kuwania nafasi hizo kutuma maombi yao mapema kupitia barua pepe This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. Cc: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Fomu za maombi zinapatikana katika tovuti ya Chama www.tamwa.org

Mwisho wa kutuma maombi ni Machi 11, 2022.

Kelvin Mtewele - Afisa Utawala, TAMWA.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Godwin Assenga, Tamwa

Kisarawe. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeadhimisha Siku ya mtoto wa kike  Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 

Maadhisho hayo yalifanyika kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na wadau wa masuala ya jinsia.

 Siku ya mtoto wa kike huadhimishwa Oktoba 11 kila mwaka ambapo mwaka huu maadhikisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo; “Imarisha uwezo wa mtoto wa kike” Tokomeza Ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kazimzumbwe iliyopo Wilaya ya Kisarawe na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye  ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe, Mussa Gama. 

Katika maadhimisho hayo watoto walipata fursa ya kufikisha ujumbe wao mbele ya mgeni rasmi kwa njia mbalimbali ikiwamo maigizo, ngonjera na risala.

Pia TAMWA kwa kushirikiana na kampuni ya Asas Diary waligawa maziwa kwa wanafunzi walioshiriki maadhimisho hayo. 

 

 

Wanafunzi toka shule mbalimbali wilayani Kisarawe wakifanya  maandamano

 

Mmoja wa wanafunzi akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa

 

Kikundi cha skauti kisarawe wakionyesha gwaride mbele ya mgeni rasmi

 

Kikundi cha maigizo kisarawe kikifanya igizo la madhara ya ukeketaji mbele ya mgeni rasmi

 

Search