Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania - TAMWA, Jumamosi 14/04/2018 kimefanya Mkutano Mkuu wa mwaka 2017 ambapo pamoja na mambo mengine, wanachama walipata fursa ya kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2017, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2018 - 2019. Mkutano huo ni wa 30 tangu kuanzishwa chma hicho na ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.

Mwenyekiti wa TAMWA Bi Alakok Mayombo, akizungumza jambo wakati wa mkutano

Mwanzilishi wa TAMWA Bi Fatma Alloo, akizungumza na wanachama wakati wa mkutano mkuu

Baadhi ya Wanachama wa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mkutano