News/Stories

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Florence Majani, TAMWA.

Ruangwa, Lindi. Kinamama katika kata ya Likunja, wilayani Ruangwa wamelaumiwa kuwa wao  ndicho chanzo cha kuvunjika kwa ndoa kila kukicha katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, kasi ya wanandoa kuachana ni kubwa na hata ile ya kuoana nayo ni kubwa hasa msimu wa mavuno.

Hayo yameelezwa jana, wakati wa mafunzo ya wanakamati za ulinzi za kata hiyo, yaliyotolewa na Chama cha Wanahabari Wanawake(TAMWA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mwalimu wa Shule ya Msingi Likunja, Maria Lilai, alisema ndoa zinavunjika kila siku kwa sababu ya mfumo wa  mwanamke kuwa na madaraka kwenye familia zaidi ya baba.

“Mfumo  wa ‘matrilinneal’ ambao unampa mama madaraka ya kuwa kichwa cha familia, ndiyo unaofanya ndoa nyingi zinavunjika. Kwa sababu wanaume wengi hawapendi kuwa chini ya mwanamke, hivyo  migogoro  mingi inaishia kwenye talaka,” alisema.

Alisema kesi zinazotolewa talaka ni za kila kukicha lakini zipo kesi ambazo wanandoa wanatengana lakini  mwanaume anakataa kutoa talaka.

“Akikataa kutoa talaka inabidi uinunue, wapo wanaume ambao hukataa kutoa talaka hadi uwape hela. Ukiwapa hela wanakupa talaka yako,” alisema.

 

Ofisa Maendeleo ya Jamii kata ya Likunja, Sarah Pongolela alisema kwa mila za Wamwera mwanaume anapooa ni lazima amjengee mke wake nyumba.

“Mara nyingi migogoro hii inaanzia kwenye mgawanyo wa mali, au pale ambapo kipato kinaongezeka,” alisema

 Alisema hakuna takwimu rasmi za matukio ya talaka kwa sababu mengi yanamalizika katika ngazi ya familia.

“Kesi nyingi zinamalizwa baada ya wanandoa kugawana mali, lakini kama kesi hiyo ina mgogoro zaidi, ndipo zinapofikishwa kwenye ofisi za kata au Bakwata au mahakamani,” alisema.

Akizungumzia kesi za talaka, Mwenyekiti wa Chama cha kinamama katika kata hiyo, Shelly Nachinuku,  alisema zipo kesi nyingi za ndoa kuvunjika lakini yeye alikuwa na maoni tofauti na Maria akidai kuwa chanzo ni wanaume.

“Kesi hizo zinaanzia kwa wanaume, mfano mwanaume akishaona amemzalisha mwanamke anamuacha, au akiona kuna watoto wengi ndani ya nyumba anamuacha na anaenda kwa mwanamke mwingine,” alisema

Alisema suala la talaka linachangiwa na wanaume kutokukaa nyumbani na kutotimiza majukumu yao  kwenye familia.

“Wanaume wanapoona msimu wa mavuno, wanazikimbia familia zao na kudai wanakwenda kuangalia mazao kumbe, wanayauza na kuanza kutumia fedha na wanawake wengine,” alisema

 Alisema hata huko shuleni imebainika kuwa wanafunzi wengi wanalelewa na mzazi mmoja au bibi  baada ya wazazi wao kuachana.

Katekisti wa Kanisa Katoliki, kigango cha Likunja, Erick Akwilambo alisema kesi hizo za wanandoa kuachana zipo nyingi katika kata hiyo na kueleza kuwa zinasababishwa na mfumo jike ambapo wanawake wanakuwa  na madaraka makubwa kwenye familia.

“Ndiyo maana hata hizi kesi za wanaume kupigwa ni nyingi, huku wanaume hawana la kusema, hata mtoto akizaliwa anakuwa ni wa ukoo wa kwa mama,” alisema

Ofisa Elimu wa Kata ya Likunja, Mwajuma Ibadi alisema sio talaka tu, bali hata ndoa nazo zinafungwa kwa wingi kama ilivyo talaka. Alisema tatizo kubwa ni kuwa wakazi wa eneo hilo wanafunga ndoa za mashindano.

“Kwa mfano, wanandoa wakiachana, basi kila mmoja atataka aoe au aoelewe tena ili kumkomoa mwenza waliyeachana,”alisema

Ibadi alisema asilimia 70 ya wanafunzi kwenye shule za msingi, wanalelewa na bibi au babu baada ya wazazi kutengana.

Alisema ndiyo maana kuna mmomonyoko wa maadili ikiwamo mimba za utotoni na elimu duni kwa kuwa watoto wengi wanakosa malezi ya wazazi wote wawili.

Mtendaji Kata ya Likunja, Hassan Kalembo alisema kesi hizo za ndoa kuvunjika zipo kwa wingi lakini hana takwimu rasmi.

“Tunapokea malalamiko hayo kila siku, lakini chanzo cha haya yote ni tamaa. Wanawake wa kabila hili(wamwera) wakiona mume amechuma mali kadhaa wanataka kuachana ili wagawane mali,” alisema.

Ofisa Maendeleo wilaya ya Ruangwa, Rashid Namkulala alisema matukio ya wazazi kutengana au kuachana ndiyo yanayosababisha malezi duni kwa watoto.

“Sisi viongozi tutaendelea kutoa elimu ya kina kwa wakazi wa eneo hili ili kesi za talaka zipungue. Tumeshuhudia kuwa watoto wanakosa malezi bora pindi tu wazazi wanapotengana,” alisema

Hata hivyo, Ofisi ya Ustawi wa Jamii ya wilaya ya Ruangwa, walisema hawana takwimu za talaka.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Ofisa Maendeleo Wilaya ya Ruangwa, Rashid Namkulala amekemea vikali Mila na desturi zinazochochea ukatili wa wanawake na watoto wilayani humo. Ameyasema hayo juzi wakati wa mdahalo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Nambilanje na ya Msingi Nambilanje. Chama Cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kimesimamia mafunzo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Kijiji cha Nambilanje na midahalo na majadiliano kwa shule za Msingi na Sekondari kuhusu Mila na desturi zinazochochea mimba za utotoni wilayani humo.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Godwin Assenga, TAMWA.

In Summary

The Tazania Media Women's Association (TAMWA) has appointed Ms Rose Reuben as the new Executive Director effectively from January 7, 2019. 

The new Director is replacing Ms Edda Sanga, whose term in office has expired after saving the Association for over three years.

The new appointed TAMWA Executive Director, Ms Rose Reuben (Right), receiving office documents from the representative of the Association’s Board Chairperson, 

Ms Judica Losai during the handing over ceremony that took place at TAMWA Office in Dar es Salaam on Friday, January 11, 2019.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Come visit the World Press Photo Exhibition 2019 on its world-wide tour showcasing the stories that matter! News photographs and stories from all over the world are seen in this exhibition. From environmental issues to sports, there will be something for everyone. This years’ exhibition is particularly special for Tanzania because one of the winning stories includes photos made by Anna Boyiazis of women having swimming lessons from instructor Kazija in Zanzibar.

OPEN DISCUSSION ON PHOTO JOURNALISM

Is telling your thoughts, perceptions and stories through photography your dream? Then this could be something for you! On Friday 1 February 2019, 15:00 pm at the Alliance Française (Dar es Salaam), Hivos together with Tamwa will organize an open discussion about photojournalism in which experts from the field will exchange their experiences and thoughts.  Even more exciting is that during this event two local photographers will be awarded with a grant of EUR 5,000 each from Voice, a partnership of Hivos and Oxfam Novib! Keep an eye on the Facebook page of the Netherlands embassy @DutchembassyTanzania and Hivos @HivosEastAfrica for more information about how to apply for the competition.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

 

Godwin Assenga, Tamwa.

Dar es Salaam. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) kinatoa pongezi za dhati kwa mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu na Mkurugenzi wa Taasisi ya Msichana Initiative, Rebecca Gyumi kwa kushinda tuzo ya Umoja wa Mataifa katika kipengele cha utetezi wa haki za binadamu kwa mwaka 2018.

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Maria Fernanda alimtangaza Gyumi pamoja na washindi wengine, Octoba 25 mwaka huu.

Washindi wengine ni marehemu Asma Jahangir , mwanasheria wa Haki za Binadamu wa Pakistan, Joenia Wapichana, mwanaharakati wa haki za watu wa jamii za pembezoni wa Brazil na  taasisi ya Front Line Defenders, inayojihusisha na ulinzi wa haki za binadamu, Ireland.

“TAMWA inaamini kuwa, ushindi wa Gyumi ni ushindi kwa watoto na wanawake wote nchini ambao haki zao zimekuwa zikikandamizwa,” anasema Edda Sanga, Mkurugenzi, TAMWA.

Wengine waliowahi kushinda tuzo hii miaka ya nyuma ni pamoja na aliyewahi kuwa mke wa Rais wa Marekani, Franklin Roosevelt, Eleanor Roosevelt, mwanaharakati wa haki za binadamu na kiongozi wa dini wa Marekani, Martin Luther King.

 Wengine ni  aliyewahi kuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na  Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu(ICRC)

 Sherehe za utoaji wa tuzo hizi zitafanyika Desemba huko New York, Marekani.

Latest News and Stories

Search