Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kimesikitishwa na kulaani vitendo na matukio ya ukatili uliopindukia unaofanywa na baadhi ya walimu kuwapiga wanafunzi bila kufuata sheria zinavyoelekeza na kupelekea baadhi yao kuathirika kisaikolojia na hata kupoteza maisha kutokana na vipigo hivyo.
Miongoni mwa matukio ya kusikitisha ni lile la tarehe 27 Agost ambapo MWANAFUNZI wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kibeta, Bukoba mkoani Kagera, Sperius Eradius (13) alifariki dunia baada ya kupigwa na mwalimu wake kwa kutuhumiwa kuiba pochi ya mwalimu.
Read more: TAMWA YALAANI UKATILI NA MAUAJI YANAYOFANYWA NA WAALIMU KWA WANAFUNZI