News/Stories

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Juni 16, 2019. Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), kinaungana na taasisi za umma na zisizo za umma zinazotetea haki za watoto  duniani katika  kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika  Juni 16 kila mwaka.

Kauli mbiu ya mbiu ya mwaka huu ni Mtoto  ni msingi wa taifa endelevu tumtunze tumlinde na kumuendeleza.

Pamoja na changamoto zinazomkabili mtoto wa kiafrika, lakini takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa ubakaji umeendelea kuwa ni janga la Taifa. 

Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na LHRC zinaonyesha kuwa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka 2018 watoto 2365 walibakwa,  idadi ambayo ni sawa na watoto 394 kwa siku.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Wakati dunia ikiadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Usalama Barabarani, viongozi wa ngazi mbalimbali nchini wametakiwa kuchukua hatua katika kudhibiti ajali za barabarani ili kuokoa maisha ya wananchi yanayopotea kila kukicha kwa kusababishwa na ajali za barabarani nchini.

Wiki ya Umoja Wa Mataifa ya Usalama Barabarani ilianzishwa kupitia Azimio la Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Oktoba 2005 ikiwa na lengo la kuboresha usalama wa barabarani duniani. Azimio hili liliitaka Tume ya Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuandaa kwa pamoja wiki hiyo. Kwa mara ya kwanza wiki ya umoja wa mataifa ya usalama barabarani iliazimishwa mwaka 2007 , ya pili mwaka 2013, ya tatu 2015, na ya nne 2017. Mwaka huu ni maadhirimisho ya tano, ambayo yanaadhimishwa kuanzia tarehe 6 mpaka tarehe 12 mwezi huu wa tano 2019.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania,(TAMWA), tumepokea kwa masikitiko kifo cha mmiliki wa kampuni za IPP nchini, Dk Reginald Mengi ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari MOAT.

 

Kifo hiki ni pigo kubwa kwa tasnia ya habari nchini, pia kwa jamii ya Watanzania hasa kwa watu wenye ulemavu.

 

Dk Mengi ameacha alama katika tasnia ya habari kwa kuanzisha vyombo vya habari na alibeba dhamana ya kuwa mlezi kwa wanahabari nchini, na alileta heshima katika tasnia hii nchini.

 

Atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika tuzo za umahiri wa habari za Ejat hasa katika maudhui kuhusu watu wenye ulemavu, ambako amekuwa akidhamini tuzo hizo.

Atakumbukwa kwa upendo wake  mkubwa kwa wenye ulemavu. Dk Mengi amekuwa muumini mzuri wa masuala ya usawa wa kijisia katika taasisi zake ambapo ametoa nafasi za ajira na za uongozi kwa wanawake na wanaume.

 

Pia Dk Mengi alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa Shirikisho la wenye Viwanda nchini.

Dk Mengi alikuwa na ndoto nyingi, mojawapo ni ya kushirikiana  na serikali kutokomeza  umaskini kama alivyoandika kwenye ukurasa wake wa twitter Machi 19, ''Ndoto yangu ni kushirikiana na serikali kutokomeza kabisa umaskini Tanzania''

 

Ulale salama Dk Mengi, tutaendelea kuyaishi maneno yako kwa mfano nukuu yake ya Januari 7 aliyotuma kupitia mtandao wake wa twitter akisema: ''Kwa unyenyekevu ninawashauri  watanzania wenzangu kuufanya mwaka 2019 kuwa mwaka wa upatanisho na msamaha, chuki ni mzigo mzito kuubeba mioyoni mwetu, kupendana ni njia peee ya kusonga mbele''.

 

Pumzika kwa amani Dk Mengi.

 

Rose Reuben

MKurugenzi TAMWA

 

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Aprili 6, 2019. Wanachama wa Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA), kimemchagua Joyce Shebe kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi ya chama hicho.

 

 Katika uchaguzi huo, pia wanachama waliwachagua wajumbe wa bodi ambao ni wanahabari Leah Mushi, Raziah Mwawanga na Halima Muselem kutoka Zanzibar.

 Kabla ya Shebe, Alakok Mayombo alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya chama hicho aliyeongoza kuanzia 2016 mpaka mwaka huu.

 Uchaguzi huo umefanyika katika mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika leo Aprili 6, 2019.

“Mimi si mzungumzaji  sana, mimi ni msikilizaji zaidi. Lakini ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa TAMWA ni wanachama. Sisi wanachama ndiyo tutakaoijenga TAMWA,”Joyce Shebe.

Shebe aliwataka wanahabari wanawake kuongeza ushirikiano kwa kuwa kwa kutumia kalamu zao wanaweza kuibadili au kuibomoa jamii.

 

Rose Reuben

Mkurugenzi Mkuu

TAMWA

Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

Mobile: 0764438084

Latest News and Stories

Search