News/Stories

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Dar es Salaam. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania, (TAMWA), kinajumuika na Waafrika wote kumpongeza Rais mpya wa Ethiopia, Sahle-Work Zewde.

 Sahle-work anakuwa Rais wa kwanza mwanamke kuiongoza Ethiopia baada ya kuteuliwa na bunge la nchi hiyo jana Octoba 25.

Taarifa iliyotumwa na TAMWA leo Oktoba 26, imesema Rais Sahle-Work, anaendelea kupeperusha bendera za wanawake waliowahi kuwa marais Afrika.

Marais wengine waliowahi kushika nyadhifa hizo ni pamoja na Ellen Johnson Sirleaf, (Liberia), Joyce Banda (Malawi) na Ameenah Gurib-Fakim, aliyewahi kuwa Rais wa Mauritius.

“Kuteuliwa kwake ni chachu ya mabadiliko zaidi kwa wanawake ambao awali hawakuaminika wanaweza kuongoza,”imesema taarifa hiyo ya TAMWA

 “TAMWA, inaendelea kuhamasisha kuwepo kwa uwakilishi wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi hapa nchini,”imesema taarifa hiyo.

Katika moja ya hotuba  zake Sahle-Work amesema; “Kukosekana kwa amani kwanza kunawaathiri wanawake, hivyo wakati wa uongozi wangu nahamasisha zaidi nafasi za wanawake katika kuleta amani.”

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Godwin Assenga, Tamwa

Kisarawe. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimeadhimisha Siku ya mtoto wa kike  Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. 

Maadhisho hayo yalifanyika kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe na wadau wa masuala ya jinsia.

 Siku ya mtoto wa kike huadhimishwa Oktoba 11 kila mwaka ambapo mwaka huu maadhikisho hayo yamebebwa na kauli mbiu isemayo; “Imarisha uwezo wa mtoto wa kike” Tokomeza Ukeketaji, Mimba na Ndoa za Utotoni.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kazimzumbwe iliyopo Wilaya ya Kisarawe na kuhudhuriwa na mgeni rasmi ambaye  ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashari ya Kisarawe, Mussa Gama. 

Katika maadhimisho hayo watoto walipata fursa ya kufikisha ujumbe wao mbele ya mgeni rasmi kwa njia mbalimbali ikiwamo maigizo, ngonjera na risala.

Pia TAMWA kwa kushirikiana na kampuni ya Asas Diary waligawa maziwa kwa wanafunzi walioshiriki maadhimisho hayo. 

 

 

Wanafunzi toka shule mbalimbali wilayani Kisarawe wakifanya  maandamano

 

Mmoja wa wanafunzi akizungumza jambo mbele ya mgeni rasmi na wageni waalikwa

 

Kikundi cha skauti kisarawe wakionyesha gwaride mbele ya mgeni rasmi

 

Kikundi cha maigizo kisarawe kikifanya igizo la madhara ya ukeketaji mbele ya mgeni rasmi

 

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Mtandao wa Wadau unaopambana na unywaji pombe kupita kiasi  – TAAnet, leo tarehe 3Machi, 2018 unaungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya kutokunywa pombe duniani ambayo kwa mara ya kwanza yanafanyika kitaifa mkoani  Dodoma.

Maadhimisho hayo yatakayoongozwa na kauli mbiu ya mwaka huu ya “Maendeleo ya Viwanda yataletwa na Udhibiti wa Unywaji Pombe kupita kiasi”  yataanza kwa maandamano yatakayopokelewa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa mkoa huo Dr. Bilinith Mahenge saa mbili asubuhi kwenye viwanja vya Chuo cha Biblia Dodoma

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Watu zaidi ya milioni 3 walifariki kutokana na matumizi mabaya ya pombe mwaka 2016. Zaidi ya robo tatu ya vifo hivi vilikuwa ni vya wanaume. Kwa ujumla, matumizi mabaya ya pombe husababisha zaidi ya asilimia 5 ya mzigo wa magonjwa duniani.

Matumizi ya pombe na athari zake ni tatizo linalozidi kukua nchini Tanzania, na linapaswa kudhibitiwa haraka iwezekanavyo. Ongezeko hili la unywaji pombe katika jamii ya watanzania TAAnet inazikumbusha  taasisi husika pamoja na Serikali kuangalia kwa hakara namna ya kudhibiti tabia hiyo ili kunusuru maisha ya vijana yanayoendelea kuharibika kila siku.

Kama wadau wa kupambana na madhara ya unywaji pombe , tungependa kuona watunga sera wanalitafutia tatizo hili ufumbuzi kwa  kuwa ufumbuzi wa ubunifu ambao utaokoa maisha, kama vile kutokomeza unywaji pombe kupindukia.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo bado haina sera/muongozo  wa pombe ukilingalinisha na Nchi jirani kama Kenya, Malawi huku Uganda wakiwa njiani kumalizia mkakati wa sera yao ya pombe.

TAAnet inapendekeza kupitiwa kwa sheria na kuweka masharti kuhusiana na matangazo, uuzaji na udhamini wa pombe pamoja na kuonyeshwa kwa onyo la athari za pombe   kwenye matangazo ya vilevi ili kupunguza matumizi yake kwa jamii.

TAAnet inaamini kwamba, endapo kutakuwa na sera ya kudhibiti matumizi mabaya ya pombe, wanaume watawajibika zaidi na kuacha matumizi yaliyopitiza ya vileo, yanayochangia unyanyasaji wa kijinsia, na badala yake kuchangia ustawi wa familia na kukuza maendeleo kwenye jamii na katika Taifa kwa ujumla.

Kupunguza matumizi mabaya ya pombe kutasaidia kufikia malengo kadhaa yanayohusiana na afya ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG), ikiwa ni pamoja na  afya ya uzazi na watoto, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa yasiyoambukizwa na magonjwa ya akili, majeraha na sumu. 

Edda sanga

Mkurugenzi Mtendaji

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
Mwandishi Wetu, Tamwa.
Kisarawe. Wadau wa maendeleo na ustawi wa jamii Wilaya ya Kisarawe wametaja  moja ya sababu zinazochangia ubakaji na ndoa za utotoni wilaya ya Kisarawe kuwa ni madereva bodaboda.
Wakizungumza leo Septemba 18 katika warsha ya wadau wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na watoto iliyofanyika wilayani humo wadau hao wamesema umbali wa shule unasababisha wanafunzi walaghaiwe na madereva bodaboda na kuishia kupata mimba au kubakwa.
Akizungumza katika warsha hiyo iliyoandaliwa na Chama Cha Wanahabari Wanawake(Tamwa) Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema ushirikiano wa wadau ni muhimu katika kumaliza ukatili huo.
"Ndiyo maana tumefurahi kwa Tamwa kuja hapa kwa sababu wanalifahamu tatizo hili kwa upana. Lakini pia tumeiwata wazee maarufu na viongozi wa dini na maofisa ustawi wa jamii pamoja na wanasheria. Nia yetu tupate suluhisho la tatizo hilo,"amesema. 
Amesema kesi nyingi hazifiki mwisho kwa sababu ya kukosekana kwa ushirikiano wa wanafamilia pindi kesi zinapofika mahakamani. 
Mkurugenzi was Tamwa, Eda Sanga amesema unyanyasaji wa  watoto unaleta simanzi na ndiyo maana chama hicho kinapaza sauti na kusema imetosha Sasa.
"Kwa kauli moja tunasema huu unyanyasaji,ukatili, utovu wa nidhamu , visasi, uonevu , dhuluma na ukiukwaji wa  haki za mtoto kiujumla utokomezwe na utokomee,"amesema. 
Tamwa inatekeleza mradi unaowezesha Wanawake na kujenga usawa wa kijinsia katika Wilaya saba Tanzania bara.

Latest News and Stories

Search