- TAMWA
- Hits: 1559
Mwandishi Wetu, TAMWA
Dar es Salaam. Wanahabari Wanawake 52 wamefanikiwa kujiunga na Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania -TAMWA mwaka huu hatua inayodhihirisha kuwa wigo wa kuripoti habari za ukatili wa kijinsia na usawa wa kijinsia, utaendelea kupanuka.
Wanachama hao wapya kutoka Tanzania Bara(26) na Visiwani(26) wamejiunga kwa ajili ya kuongeza wigo katika harakati za kuondoa mifumo yote ya ukatili wa kijinsia na kuwawezesha kitaaluma wanahabari wanawake nchini.
Akizungumzia kujiunga kwa wanahabari wapya katika chama hicho Mkurugenzi wa TAMWA, Rose Reuben amesema kujiunga kwa wanahabari hao kunaongeza jitihada za kutetea haki za wanawake na watoto zenye mrengo wa kijinsia.
“Wakati huu tunapaswa kuwa na taarifa mbalimbali zenye mrengo wa kijinsia zitakazosaidia wananchi , watunga sera na jamii kwa ujumla kuelewa kwamba jamii yetu inahitaji sera na taarifa za kiuchumi na kijamii.”alisema
Reuben amesema, wanahabari ambao hawajajiunga wakati ni sasa ili kuungana pamoja katika kuinuana kitaaluma, kuungana na wanawake kutetea haki za wanawake na watoto na kuongeza wingo wa wanawake kuungana na kuwa na sauti moja.
Amesesitiza faida za kuwa mwanachama wa TAMWA ni kupata mkopo wa kujiendeleza kitaaluma katika stashahada ya kwanza au ya pili na baadae kurudisha mkopo huo bila riba.
“Pia kuna mafunzo ya kubadilishana taaluma (exchange program) zinazopatikana nchini na hata nje ya nchi, kumuongezea uwezo wa kitaaluma kwa mafunzo yanayotolewa na TAMWA kwa wanahabari, pamoja na kuandika taarifa mbalimbali za kijamii ambazo zitaweza kumuongeza zaidi katika taaluma yake,” alisema
Ili kupitishwa kuwa mwanachama unatakiwa kuwa na Diploma ya Habari, uzoefu katika fani ya uanahabari usiopungua miaka mitatu na kisha kupata wadhamini watatu ambao ni wanachama wa TAMWA.
Mwanachama mpya wa TAMWA, Bupe Mwakyusa, Mwandishi wa Mlimani TV ameelezea matarajio yake baada ya kuchaguliwa kuwa mwanachama kuwa ni pamoja na kupata uzoefu zaidi katika taaluma ya habari na kushiriki katika miradi mbalimbali ya masuala ya kijinsia.
“Kilichonishawishi zaidi kujiunga TAMWA nikiwa mwanahabari ni kujifunza zaidi kuhusu taaluma ya habari pamoja na kupata maarifa zaidi kutoka kwa waliofanikiwa katika taaluma ya habari kupitia TAMWA, pia naamini kupitia TAMWA ntafika mbali zaidi”, alisema
TAMWA ilianzishwa mwaka 1987 na wanahabari wanawake nchini na mpaka sasa kina wanachama zaidi ya 100.
MUUNGANO WA ASASI ZA KIRAIA ZINAZOSHAWISHI MABORESHO YA SHERIA YA USALAMA BARABARANI
TAREHE: 23 MEI 2020
UKUMBI: PIUS MSEKWA DODOMA
KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI
Ndugu Waheshimiwa Wabunge;
Ndugu wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Ya Nchi;
Ndugu wawakilishi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto;
Ndugu Wakurugenzi Asasi za Kiraia zinazoshawishi Maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani;
Ndugu Waandishi wa habari na wadau wote wa Usalama Barabarani, Mabibi na Mabwana;
Ndugu Waandaaji wa hafla hii Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Mwananchi Communication; - Habari za asubuhi.
HOTUBA
YA
BI ROSE REUBEN - MKURUGENZI MTENDAJI (TAMWA)
KWENYE
KONGAMANO LA USALAMA BARABARANI
MADA: USALAMA BARABARANI KWA AFYA NA MAENDELEO YA UCHUMI
UKUMBI: UKUMBI WA BUNGE PIUS MSEKWA- DODOMA
TAREHE: 23 MEI 2020
"Mtandao wa Usalama Barabarani Tanzania ni nini?. Kitu gani mtandao umefanya kuhusiana na Usalama barabarani?. Dhumuni kuu ni nini?"
Ndugu Mgeni Rasmi, Waheshimiwa Wabunge, wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani Ya Nchi, wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Viongozi wa Serikali, Wawakilishi Asasi za Kiraia zinazoshawishi Maboresho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Washirika wa Maendeleo, Wanahabari na Vyombo vya habari mliopo, Waathirika wa ajali za barabarani, Wageni waalikwa Mabibi na Mabwana,
Ni heshima kubwa kwangu kutoa hotuba hii, kwa niaba ya mtandao katika kongamano hili muhimu.
Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai na kutuwezesha kukutana hapa siku ya leo. Napenda kuwapongeza TAMWA na Mwananchi communications kwa maandalizi bora ya mkutano huu.
Napenda pia kulishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali kuwa mwenyeji wa hafla hii.
Napenda pia kushukuru na kutambua juhudi kubwa za wajumbe wa Mtandao ambao wamefanya kazi kwa bidii kutayarisha hafla hii, haswa katika kufikia adhma ya
Naomba nianze kwa kutoa historia fupi ya mtandao huu wa asasi za kiraia unaoshawishi maboresho ya sheria ya usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kazi na mafanikio yake;
Mabibi na Mabwana,
Shirikisho la Usalama Barabarani Tanzania (CSO's) lilizinduliwa mnamo Mei 2016, na wanachama sita tu chini ya uratibu wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), lakini umeongezeka hadi leo hadi wanachama wapatao kumi na tano ambao ni pmaoja na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA), Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA), Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), Amend Tanzania, Shirikisho la Vyama vya Watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA), Taasisi ya Taifa ya Usafirishaji (NIT), Tanzania Media Foundation (TMF), Safe Speed Foundation, Women Legal Aid Centre (WLAC), WILDAF, Mwanza Youth and Children Network (MYCN), Media Space Tanzania, pamoja na watu binafsi wenye utaalamu na mapenzi na usalama barabarani.
Wajumbe wa umoja huo wamekuwa wakifanya kazi na Serikali (haswa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Uchukuzi na idara / mashirika chini ya wizara hizi), Shirika la Afya Duniani (WHO), Wabunge na watendaji wengine kuunga mkono utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Sheria, haswa juu ya mabadiliko ya sera kwa marekebisho kamili ya Sheria ya Sheria ya Usalama Barabarani (RTA). Sekretarieti ya Ushirikiano kwa sasa upo chini ya usimamizi wa TAWLA.
Mtandao huu ulianzishwa kwa malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuwa na sauti ya pamoja katika kuendesha kampeni ya kushawishi maboresho ya sheria ya usalama barabarani pamoja na kuongeza uelewa kwa umma juu ya masuala mbalimbali ya usalama barabarani.
vilevile mtandao huu uliundwa kwa lengo la kuwa kama kiungo kati ya watumiaji wa barabara pamoja ba viongozi wa serikali/watunga sera ili kushawishi kuwepo kwa mfuno wa kisheria na kisera unaoendana na viwango vya kimataifa.
Mtandao umerekodi mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa kwa watumiaji wa barabara juu ya ukubwa wa tatizo hasa kwenye viashiria vitano vinavyochangia ongezeko ajali.
Mtandao umefanya kazi kwa karibu na kamati mbalimbali za bunge, hii ilipelekea wao kushawishika na kuamua kuanzisha mtanao wa kibunge unaojihusisha na masuala ya usalama barabarani ambao una takribani ya wabunge 120.
Mtandao unafanya uchechemuzi juu ya mfumo bora wa kisheria juu ya usalama barabarani ili kuhakikisha kuwa ajali za barabarani zinapungua, ikiwa ni pamoja na majeraha yatokanayo na ajali za barabarani pamoja na vifo. Pia shirikisho linatetea na kupigania uwepo wa Sheria ya Usalama Barabarani (RTA) ya mwaka 1973. Kuna mapungufu ambayo yalitambuliwa katika Sheria ya Usalama Barabarani (RTA) na kwamba ikiwa yataboreshwa, ajali za barabarani zitapungua, idadi ya majerahi na vifo vitokanavyo na ajali za barabarani zitapungua.
Mapungufu yaliyotambuliwa yanahusiana na visababishi vitano hatarishi ambavyo ni; Mwendo kasi, Matumizi ya vilevi wakati wa kuendesha chombo cha moto, Kutotumia kofia ngumu (helmet) kwa abiria na dereva wa pikipiki, Kutokufunga mikanda wakati wa safari, na kutotumia vizuizi vya watoto.
Kwa mara nyingine ninawashukuru na kuwapongeza wote ambao wamefanikisha tukio hili. Ni matumaini yangu kuwa maazimio yote tutakayoafikiana hapa katika kongamano hili, yatafanyiwa kazi na kuja na njia ambazo ni bora na sahihi zaidi katika kupunguza ajali za barabarani .
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.!
“Ahsanteni sana kwa kunisikiliza”
Aprili 11, 2020. Wakati huu ambapo dunia nzima inapambana na ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na virusi vya Corona, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinawakumbusha wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kufuata miongozo ya kutekeleza majukumu yao kwa kujilinda na maambukizi ya ugonjwa huu, na kutumia zaidi teknolojia ya mawasiliano. Ugonjwa wa Covid-19 unaweza kumuathiri mtu yeyote, hivyo wanahabari, wamiliki wa vyombo vya habari na wadau wote wa habari wanapaswa kukubaliana na mabadiliko ya kiutendaji kazi yatakayowaepusha dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu. TAMWA inawashauri wanahabari na wamiliki wa vyombo vya habari kujikita katika kutumia maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano kupata habari badala ya kwenda katika mikusanyiko isiyo ya lazima kwani taarifa zinaweza kutumwa kimtandao au mahojiano kwa njia ya simu. “Bila shaka hofu ya ugonjwa wa Covid 19 itabadili mfumo wa utendaji kazi wa tasnia ya habari kama taasisi inayohudumia jamii na kuanza kujiona kuwa na wao pia ni sehemu ya jamii,” TAMWA tunathamini usalama wa wanahabari kwa kuwa sisi ni sehemu na mdau wa vyombo vya habari ambavyo vimekuwa chanzo cha ufikishaji wa taarifa za kutetea haki za wanawake na watoto zenye lengo la kuwa na Tanzania inayoheshimu misingi ya usawa wa jinsia. Wanahabari wanaoripoti kuhusu COVID-19 na wanahabari wengine, wanashauriwa kufanya maandalizi kabla ya kwenda katika mikutano, kwa kufuata mbinu za kujikinga na maambukizi.
Aprili 7, 2020. Wakati dunia nzima ikigubikwa na mshtuko kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinapenda kuihadharisha jamii juu ya ongezeko la ukatili wa wanawake na watoto unaoweza kukithiri wakati wa janga la ugonjwa huu.
“Watoto wapo nyumbani wakati huu ambapo serikali imezifunga shule, lakini iwapo wazazi na walezi hawatakuwa makini basi huenda wakaathirika na ubakaji na mimba za utotoni katika kipindi hiki ambacho macho na masikio yapo katika kudhibiti virusi vya Corona,”
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia watoto(UNICEF) linasema, ukatili wa watoto aghalabu hufanyika nyumbani, mtoto akielekea au akitoka shule wakati anapokuwa peke yake bila msaada.
TAMWA inaipongeza serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kufunga shule ili kupunguza msongamano unaoweza kusababisha maambukizi, hata hivyo ni muhimu kuihadharisha jamii kuhusu ukatili wa kijinsia na ule wa watoto unaoweza kuongezeka wakati huu.
Endapo wazazi/walezi hawatawasimamia vizuri watoto katika kipindi hiki cha siku 30 zilizotolewa na serikali kupitia Waziri Mkuu, basi tunaweza kutengeneza kizazi kingine kilichoathirika na ukatili wa aina mbalimbali ikiwamo ubakaji, ulawiti na mimba zisizotarajiwa.
Kwa mfano, Ripoti ya UNICEF 2016 inaonyesha kuwa, wakati wa mlipuko wa Ebola Afrika Magharibi 2014 hadi 2016, ulisababisha ongezeko la ajira kwa watoto, ukatili kwa wanawake na watoto na mimba za utotoni. Kwa mfano, mimba za utotoni nchini Sierra Leone ziliongezeka kufikia 14,000 kutoka 7,000.
“Ni muhimu kwa wazazi na walezi kuwalinda watoto na virusi vya Corona lakini wakati huo huo tuangalie madhara wanayoweza kuyapata watoto wa kike na wa kiume wanapokuwa nyumbani au mitaani”
Tunapaswa kujiuliza iwapo watoto wetu wapo salama wawapo nyumbani au mitaani wanapotembea wakati huu wa likizo ndefu. Je, Mafataki hawawanyemelei? Je ndugu na jamaa wanaobaki na watoto hawa wanawalinda au wanawaharibu? Je watoto hawa hawatakuwa katika hatari ya kuozwa mapema?
Si hivyo tu, janga hili la Corona linaathiri zaidi wanawake kwani shule zinapofungwa, mzigo mkubwa wa malezi unawaangukia kinamama nyumbani ambao ndiyo walezi wakuu wa familia.
Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) zinaonyesha kuwa, dunia nzima, asilimia 70 ya watoa huduma za jamii na za afya ni wanawake. Majukumu haya huwaweka mstari wa mbele katika utoaji wa huduma, Je katika janga hili la Covid-19, wanawake wanalindwa ipasavyo wasidhurike?
TAMWA inaiomba serikali, wadau na watunga sera kwanza, kutosahau hatari nyingine zinazoweza kuwapata wanawake na watoto katika kipindi cha janga la Covid-19.
Pili, wadau wa afya, elimu na watoto kutoa mafunzo kuhusu namna ya kujilinda na ya kuripoti kuhusu ukatili kwa watoto wakati huu wa mlipuko.
Tatu, kuongeza upatikanaji wa taarifa na misaada mingine kwa watoto.
Nne, kubuni mfumo wa kuwapa watoto elimu wawapo nyumbani.
Tano, wahudumu wa afya wanawake wawekewe mazingira salama ya kutoa huduma ili wasiathirike.
Sita, wazazi na walezi kuimarisha ulinzi na kuzuia matembezi yasiyo ya lazima kwa watoto.
Rose Reuben
Mkurugenzi Mtendaji,
TAMWA.
CALL FOR CONSULTANCY SERVICES TO CONDUCT SRHR REPORTING SURVEY IN THE MEDIA OF TANZANIA
Mkurugenzi TAMWA aonya wanafunzi na matumizi ya mitandao ya kijamii