Gallery

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimethibitishwa na kutangazwa kuwa Sekretarieti mpya ya Mtandao wa Ushiriki wa  Wanaume na Wavulana katika masuala ya Jinsia (Men Engage Tanzania MET).

TAMWA imepewa jukumu hilo baada ya kufanyiwa tathmini na Shirika la Wanaume na Wavulana katika masuala ya Jinsia (Men Engage Afrika MEA) mapema mwaka huu baada ya Mtandao huo nchini kuratibiwa na shirika la Child Diginity Forum (CDF) kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. 

Katika jukumu hilo TAMWA itaendeleza historia yake ya utetezi wa haki za binadamu kwa mrengo wa kijinsia kwa kuwahusisha wanaume na wavulana kupinga ukatili na kuhamasisha mawasiliano kuanzia ngazi ya familia, jamii, kitaifa hadi kimataifa. 

Pamoja na hilo, TAMWA imepewa jukumu la kufanya kazi pamoja na mashirika wanachama katika kujengeana uwezokuhamasisha haki, usawa,na kupambana na ukatili kijinsia.

Mtandao wa MEA una mashirika wanachama takribani 31nchini huku ukiwa na jumla ya mashirika wanachama zaidi ya 400 kutoka  Afrika, Amerika ya Kusini,Amerika ya Kaskazini, Asia na Bara la Ulaya.

Mkurugenzi Mtendaji

TAMWA

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Dar es Salaam, Novemba 14, 2025. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania(TAMWA) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani(GIZ) leo wanazindua mradi wa ‘Sauti Zetu’  wenye lengo la kupaza sauti ili kuzuia, kupunguza ukatili wa kijinsia  na kutoa elimu kwa kutumia vyombo vya habari .

Sambamba na uzinduzi huu, TAMWA na GIZ kwa pamoja tunapaza sauti zetu ili kuwasaidia wanawake na watoto dhidi ya ukatili wa kidijitali.

Haya yote yanafanyika wakati dunia inaelekea katika kuadhimisha Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, kuanzia Novemba 25 hadi Desemba 1.

Hivyo basi, TAMWA tunaamini kuwa, uzinduzi wa mradi huu unafanyika huku kukiwa na haja kubwa ya kuwasaidia wanawake na watoto dhidi ya madhila ya ukatili unaofanyika mtandaoni.

Ukatili wa mtandaoni unawaathiri wanawake na watoto  sambamba na makundi mengine kwa kiasi kikubwa kwani kundi hili bado halina uelewa wa kutosha wa kujilinda na kulinda taarifa zao. 

TAMWA kwa uzoefu na kwa tafiti tulizowahi kufanya tumebaini kuwa faida na hasara za matumizi ya dijitali ni sawa na shilingi yenye pande mbili kwani wanawake na watoto wanatumia vifaa vya kidijitali na kupata faida lukuki lakini kwa upande mwingine mitandao ya kidijitali inawaathiri. 

Na leo tunayo furaha kubwa kuzindua mradi huu adhimu wa ‘Sauti Zetu’ wakati ambapo tumebakiza siku chache tu kabla ya  kuadhimisha Siku hizi 16 za Kupinga ukatili wa kijinsia. 

Tukirejea kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambayo mwaka huu inasema: ‘Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia 2025: Maliza ukatili wa kijinsia kupitia majukwaa ya kidijitali kwa wanawake na wasichana wote’.

TAMWA tunasisitiza kuwa wanawake na watoto wanapaswa kulindwa dhidi ya ukatili huu wa kidijitali.

Kwani tumeshuhudia madhara ya afya ya akili na ya kimwili yanayosababishwa na matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii. 

Kumekuwa na juhudi za dhati za serikali, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na wanaharakati wa masuala ya jinsia.

Kwa mfano, Mkataba wa Kidijitali wa Kimataifa wa 2024 (Global Digital Compact)uliweka viwango vya kwanza vya Umoja wa Mataifa kuhusu usalama wa kidijitali na utawala wa akili bandia (AI governance).

Mwezi Desemba 2024, nchi Wanachamazilipitisha Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Uhalifu wa Mtandaoni (UN Cybercrime Convention), chombo cha kwanza cha kisheria cha kimataifa chenye athari katika kukabiliana na ukatili wa kidijitali.

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN General Assembly)pia ulipitishaazimio kuhusu Ukatili Dhidi ya Wanawake katika Mazingira ya Kidijitali mwaka 2024, likizitaka nchi kuchukua hatua za haraka na madhubuti za kuzuia na kutokomeza ukatili wa kidijitali, pamoja na kuimarisha udhibiti na uwajibikaji wa majukwaa ya mtandaoni.

Lakini bado TAMWA imeona kuna uelewa mdogo juu ya matumizi sahihi ya majukwaa ya kidijitali hali inayochagiza madhara kwa kundi hili la wanawake na watoto. 

Kwa mfano, kusambaza picha au video za faragha bila ridhaa, mara nyingi hutumika kuwaaibisha, kuwabambikizia makossa, au kuwatala wanawake na wasichana. 

Mengine ni kufichua taarifa binafsi kwa kuweka namba ya simu, mahala pa kazi au sura ya mwanamke mitandaoni kwa lengo la kumtisha. 

Lakini pia kuna ukatili wa mitandaoni ambapo watu huunda akaunti bandi kwa kutumia jina au picha ya mwanamke ili kuharibu sifa yake au kudanganya watu wengine.

Ukatili mwingine ambao kimsingi unafanyika sana hapa nchini ni kauli za chuki au maudhui ya chuki ambapo watu huandika au kutamka maneno ya matusi yanayochochea ubaguzi au ukatili dhidi ya wanawake na wasichana. 

Mengine ni wadhalilishaji kutumia vitisho kwa kusambaza picha au video za faragha na kisha kudai pesa au upendeleo wa kingono. 

Wasichana wadogo wanaotumia mitandao kama Whatsap, Tiktok na Snapchat wapo katika hatari kubwa zaidi.

Madhara ya ukatili huu ni makubwa kwani vifo, kukosa haki, kutengwa na athari kubwa za kisaikolojia zimewakumba wanawake na wasichana.

Hivyo basi TAMWA tunapozindua mradi huu na tunapoelekea katika kuadhimisha Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, tunapaza sauti zetu kwa kufundisha na kukemea vitendo vyovyote vya ukatili wa kijinsia kwa njia ya kidijitali.

Katika kuanza utekelezaji wetu, tumeandaa ‘ Mwongozo wa Kanuni 10 za Kujilinda na Ukatili wa Kidijitali’

Uzinduzi wa Mwongozo huu unakwenda sambamba na safari yetu ya ‘Kupaza sauti’ ili kupunguza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto kupitia vyombo vya habari

KUHUSU MRADI WA SAUTI ZETU

Mradi huu unalenga kutumia vyombo vya habari kama nyenzo ya kuelimisha jamiikuhusu masuala ya Ukatili wa Kijinsia (GBV),ikiwemo kueleza maana ya GBV, chanzo chake katika jamiina kutoaelimu kuhusu huduma zilizopo kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.

Kupitia utoaji wa ujumbe muhimu kuhusu masuala ya GBV, mifumo ya kisheria, haki za waathirika na njia za kupata hakimradi huu utawawezesha waathirika kupataufahamu wa haki zao na huduma za msaada zilizopo.

Aidha, mradi huu utalenga kuongeza uelewa wa umma, kupinga mila na desturi kandamizina kuhamasisha wadau mbalimbali kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Mradi huu unatekelezwa katika mikoa minne ya Tanzania Bara, ambayo ni Dar es Salaam (Kinondoni, Temeke), Dodoma (Chamwino, Bahi) na Tanga (Lushoto na Tanga Mjini). 

Vyombo vya habari vitakuwa ndicho chombo kikuu cha kufikisha taarifa, kuongeza uelewa na kutumika kama daraja kati ya jamii, asasi, waathirika na jamii nzima.

User Rating: 5 / 5

Star ActiveStar ActiveStar ActiveStar ActiveStar Active

Chama Cha Waandishi Habari Wanawake (TAMWA) kimepewa mafunzo ya siku nne kwa ajili ya kujengewa uwezo kuhusu   masuala ya usalama wa kimtandao  ili kuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi na kwa usalama.

 
Mafunzo hayo yametolewa na taasisi ya Jamii Forum Jijini Dar-es-Salaam ambayo kwa sasa inasimamia masuala ya demokrasia, utawala bora na usalama wa kimtandao. 
 
 Mkurugenzi wa Jamii Forum Maxence Mello amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa TAMWA kwani taasisi hiyo inahitaji kuwa na ujuzi wa masuala ya usalama wa kimtandao ili kuepusha kupoteza takwimu muhimu.
 
Mello amesisitiza umuhimu wa mafunzo ya usalama wa kimtandao kwa kuwa dunia ya sasa imekuwa kwa kasi kiteknolojia hivyo kila wakati inapaswa kupewa mafunzo ili kuwa katika usalama zaidi.
 
“TAMWA na Jamii Forum tuna uhusiano wa muda mrefu na hivyo daraja hili liwe imara na tuendelee kuwasiliana na ikiwezekana muwe mabalozi wetu’’ alisema Mello
 
Kwa upande wake, Mkufunzi wa Mafunzo hayo, John Kaoneka   ameiomba TAMWA kuboresha vifaa vyake ili viwe katika mfumo wa kisasa zaidi kwa ajili ya kuboresha mawasiliano na usalama wa takwimu na taarifa muhimu.

User Rating: 1 / 5

Star ActiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Dar es Salaam, Novemba 5, 2025.Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kinatoa pole za dhati kwa Watanzania wote waliopata madhila kwa ndugu, jamaa, Tasnia ya Habari na marafiki kutokana na vurugu zilizojitokeza wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

TAMWA inawapa pole maalum familia zote zilizopoteza wanawake, watoto, na wanahabari, sambamba na wale wote walioumia au kuathirika kwa namna yoyote kutokana na matukio hayo ya kusikitisha.

Wakati Taifa likipita katika kipindi hiki kigumu, TAMWA inaungana na Watanzania wote wanaofanya jitihada za kuijenga upya hali ya utulivu, mshikamano na amani nchini. Tunaendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda utu, kuheshimu haki za binadamu, na kudumisha mazungumzo ya amani kama nguzo ya taifa letu.

Dkt. Rose Reuben
Mkurugenzi Mtendaji.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive
Machi 18, 2021. Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
 
TAMWA inaungana na watanzania wote kuomboleza kifo cha kiongozi  huyo mahiri, Rais John Pombe Magufuli. 
Kwa niaba ya wanachama wa TAMWA, bodi ya TAMWA, Wanahabari, Wanawake, na wapigania haki za jinsia, tunatoa pole kwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu,  familia ya Rais Magufuli, Mama Janeth Magufuli viongozi wa serikali na watanzania wote kwa kumpoteza kiongozi wa nchi. 
 
TAMWA inaomboleza msiba huu kwa kukumbuka mafanikio yaliyofanywa na Rais Magufuli katika kipindi cha uongozi wake tangu mwaka 2015. 
 
Rais Magufuli alikuwa na juhudi katika kujenga miundombinu ambayo kwa kiasi kikubwa ilisaidia kumkomboa mwanamke kuanzia ngazi za chini. 
Miundombinu aliyojenga kuanzia ya maji, barabara na mingineyo, ilikuwa inalenga kumkomboa mwanamke, kumtua mama ndoo kichwani na kumsaidia mjasiriamalia mwanamke kufanya shughuli zake kwa umakini na ufasaha, 
Aliwahi kusema kuwa, katika wizara inayomnyima raha  ni wizara ya maji, na hivyo akaamua kuimairisha eneo hilo ili kuhakikisha adha ya maji inatoweka. Kwa kufanya hivyo alimsaidia sana mwanamke wa kijijini na mjini, mwanamke na mtoto wa kike, kwa sababu ukosefu wa maji ulichangia kwa kiasi kikubwa ukatili wa kijinsia, ukosefu wa masomo na ufinyu wa kipato. 
 
Rais Magufuli alikuwa akijipambanua kuwa rais wa wanyonge na kweli alijitahidi kuimarisha miundombinu ya maji, umeme na kuwatazama wajane waliodhulumiwa kwa namna moja au nyingine, kuondoa riba kwa mikopo ya wanawake ya Halmashauri. 
 
TAMWA tulitamani Rais Magufuli, akamilishe kipindi chake  cha uongozi ili Watanzania tupate hasa kile alichodhamiria kukamilisha, kwa sababu alikuwa na maono makubwa.
TAMWA itamkumbuka Rais Magufuli kwa kuwa rais wa kwanza kumteua mwanamke kuwa Makamu wa Rais. 
Kwa hili aliweka historia nchini, ya kuwepo Makamu wa kwanza wa Rais mwanamke, hata kama hatujaifikia ile asilimia 50 kwa 50 ya ushiriki wa wanawake katika siasa na uongozi, 
 
Rais Magufuli atakumbukwa kama kiongozi aliyekuwa anatamani kuwakomboa wananachi kwa ujumla na sio kuwepo kwa mafanikio ya mtu mmoja mmoja. 
 
Mungu ailaze roho ya Hayati John Pombe Magufuli Mahali pema Amina!
 
Rose Reuben
Mkurugenzi Mtendaji 
TAMWA.

Star InactiveStar InactiveStar InactiveStar InactiveStar Inactive

Mwandishi wetu, Dar es salaam.

Mpiga picha wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Aika Kimaro, ameibuka mshindi wa pili katika shindano la kupiga picha za habari.

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo alikuwa mpiga picha wa kujitegemea, Imani Isamula ambaye aliibuka kidedea kwa kura 57 dhidi ya kura 43 alizopata Aika.

Washindi hao walitangazwa juzi jijini Dar es Salaam katika mdahalo katika mdahalo ulioandaliwa na Ubalozi wa Netherland katika mwendelezo wa maonyesho ya picha (World Press Photo 2018) ambayo yanaendelea.

Imani aliibuka kidedea kutokana na picha zake za walemavu wa miguu ambapo mlameavu mmoja ni mwanamke ambaye amekimbiwa na mume wake na kuachiwa watoto ambao anawalea peke yake.

Katika picha nyingine mlemavu wa kiume ambaye licha ya ulemavu wake anaonekana kujishughulisha na shughuli za uvuvi wa samaki.

Kwa upande wa Aika moja kati ya picha zakie mbili zilizoshinda, inamuonyesha mwanamke aliyebeba mzigo wa magunia mawili yaliyofungwa kwa kamba yakiwa na chupa tupu za plastiki huku amebeba mtoto mgongoni anavuka barabara.

Akifafanua kuhusu picha hizo, Aika alisema mama huyo licha ya kuwa na shuguli nyingi nyumbani ambazo hazimuingizii kipato ameamua kumbeba mtoto wake mgongoni na kuamua kuingia mtaani kujitafutia chochote kwa ajili ya watoto wake.

“Katika picha ya pili, hawa ni watoto wanaonekana wakiwa na magunia wanaokota makopo na chupa za maji ili wakauze, picha hii inazungumza mengi, kwanza hawa ni watoto ambao wamekosa haki zao za msingi kama haki ya kusoma na haki ya kucheza,” alisema Aika.

Search