- TAMWA
- Hits: 343
PRESS RELEASE
March 27,2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO MKUU WA TAMWA 2014 JUMAMOSI
Zaidi ya Wanachama 100 wa Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA Jumamosi tarehe 28th Machi, 2015 wanafanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka 2014 ambapo pamoja na mambo mengine wanachama watapata fursa ya kutathmini kazi zilizofanyika mwaka 2014, na utekelezaji wa mpango mkakati wa 2015-2021. Mkutano huo utaanza saa 2:00 asubuhi katika ofisi za chama zilizoko Sinza Mori, Dar es Salaam.
Mkutano huo utakaoanza na mafunzo Ijumaa tarehe 27th Machi mwaka huu utawapa fursa wanachama kujadili mafanikio yaliyopatikana kwenye mpango mkakati wa miaka mitano iliyopita (2009 -2014) pamoja na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji ambapo pia watamchagua Mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwepo kumaliza muda wake.
Aidha Siku ya Jumamosi baada ya mkutano huo wanachama watajumuika pamoja katika hafla ya kuchangia mfuko wa shughuli za TAMWA (Gala Dinner) ambazo ni pamoja na kupiga vita vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto itakayofanyika jioni katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Mkutano mkuu wa TAMWA ndicho chombo cha juu chenye mamlaka ya kurekebisha katiba yake, kuingiza wanachama wapya, kuchagua viongozi, kupitisha ripoti za mwaka na kutoa maamuzi kuhusu mipango na mikakati ya chama kuhusu utetezi.
Valerie N. Msoka
Mkurugenzi Mtendaji
PRESS RELEASE
TAMWA ANNUAL GENERAL MEETING 2014.
Over 100 TAMWA members will on Saturday, 28th March, 2015 sit for Annual General Meeting (AGM) and among other things get an opportunity to evaluate the 2014 performance and the implementation of the 2015-2021 strategic plan. The meeting will begin at 8.00am at its offices Sinza Mori, Dar es Salaam.
The AGM which will begin with a seminar on Friday, 27th March this year shall give members an opportunity to discuss the progress made in the last five years of strategic plan (2009-2014) and the challenges occurred during the implementation and chart the way forward for betterment of the association. They will also elect the new chairperson for the organisation as the current chairperson’s term has ended as per TAMWA’s constitution.
Furthermore on Saturday after their AGM, members shall converge together in the Fundraising for the TAMWA activities (Gala Dinner) that includes the fight against all acts of Violence Against Women and Children which will be held in the evening at Serena Hotel, Dar es Salaam.
The AGM is the supreme organ of TAMWA which among other things, amend its constitution, admits new members, appoint new leaders, approves the Annual and Financial Audited reports of the previous work and also make decisions about programs and strategies on advocacy.
Valerie N. Msoka
Executive Director
March 20,2015
TAMWA KUKUTANA NA WAHARIRI KUJADILI UKATILI UNAOSABABISHWA NA ULEVI WA POMBE KUPINDUKIA
Na Mwandishi wetu.
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini- TAMWA leo tarehe 20 Machi, 2015 saa 3:00 asubuhi kinakutana na Wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali kujadili mikakati kwa kutumia vyombo vya habari ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyosababishwa na unywaji pombe kupindukia.
Mkutano huo wa TAMWA na Wahariri utajadili njia zitakazotumika kwa jamii ili kuweka uelewa wa madhara ya unywaji pombe kupindukia kwani unachangia ongezeko la vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na kurudisha maendeleo nyuma.
Akizungumza; Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi – CRC kilichoko ndani ya TAMWA Bi. Gladness Munuo amesema kwa mwaka mzima wa 2014, kilipokea kesi 107 za vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyosababishwa na ulevi wa pombe kupindukia ambapo kati ya hizo wanawake walikuwa 80, wanaume 22 na watoto walikuwa ni watano.
Aidha katika mkutano huo; Wahariri watajadili mbinu jinsi ya kukuza uelewa wa jamii juu ya madhara ya unywaji pombe kutokana na kuwa baadhi ya wanaume wamekuwa wakitelekeza familia zao na kuacha wanawake wakihangaika na watoto.
Akizungumza na mwandishi wetu, Bi. Munuo alisema vyombo vya Habari vikitumika katika kutoa elimu ya madhara ya unywaji pombe hasa kwa ukatili ambao umekuwa ukifanywa kimya kimya vinaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo ndani ya jamii
Bi Munuo aliutaja ukatili unaofanywa kimya kimya kuwa ni wa kingono, ubakaji na vipigo ambao unafanyika ndani ya familia huku idadi ya wanawake na watoto kutelekezwa ikiendelea kuongezeka.
Aidha baadhi ya wanandoa wamekuwa wakitumia kilevi kupindukia na kusababisha wengine kushindwa kuwahudumia watoto wao ki - afya, kukosa chakula na mahitaji mengine kama ada za shule hali ambayo husababisha taifa kupoteza nguvu kazi. Mkutano huo ni mwendelezo wa mikakati ya kupinga vitendo vya ukatili unaosababishwa na nywaji pombe kupindukia katika kukuza uelewa wa jamii ili kuwezesha kutoa taarifa za matukio hayo pamoja na madhara ya kiafya na maendeleo kupitia Habari, vipindi vya redio na televisheni.
February 24,2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UBALOZI WA KANADA KUMTUNUKU MKURUGENZI MTENDAJI WA TAMWA KUWA BALOZI WA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI
Ubalozi wa Canada nchini Tanzania kwa mara ya kwanza utamkabidhi Muurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Msoka kuwa balozi wa kampeni ya kupinga ndoa za utotoni (CEFM).
Kwa mujibu wa Ubalozi huo, tukio hilo litafanyika leo, Februari 24, 2015 katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana. Hafla hiyo itahudhuriwa, miongoni mwa watu wengine, na Katibu Mkuu Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe, Balozi wa Canada nchini Tanzania, Alexandre Lévêque, Msaidizi wa Balozi wa Canada anayehusika na masuala ya kisiasa, Eric Bertram, na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa na vyombo vya habari.
CEFM inatambua mchango uliotolewa na mtu ambaye ametumia jitihada na muda wake mwingi katika kutetea haki za watoto na ambaye amekuwa akiunga mkono harakati za kuhakikisha taifa letu linakua mahali salama kwa watoto hasa watoto wa kike katika kizazi cha sasa na kijacho.
Kutokana na uzoefu wake wa kupigania haki za biandamu hasa haki za wanawake na watoto, Valerie, ameifanya TAMWA kuwa jina la kukumbukwa katika kuleta usawa na haki za wanawake na watoto. Majukumu yake ya hivi karibuni ni pamoja na:
Mbunge katika Bunge Maalum la Katiba: Alifikisha masuala ya ndoa za utotoni nchini Tanzania katika bunge hilo na haja ya kuingiza umri wa motto unaotambulika kisheria katika katiba. Hii ilisababisha kamati za Bunge hilo kupendekeza umri wa motto kikatiba kuanzia 0 hadi miaka 18.
Mjumbe wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalum la Katiba: Aliweza kutetea masuala ya usawa ndani ya kamati ikiwa ni pamoja na haki ya kumlinda mtoto wa kike na wanawake dhidi yya mila potofu ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni, ukeketaji, haki ya kumiliki ardhi na uongozi.
Mjumbe wa Mtandao wa Kupinga Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN): Aliwezesha kuundwa kwa ukanda huru wa kukomesha ndoa za utotoni nchini Tanzania (Agosti 2014) kwa kuwa mwezeshaji wa tukio hilo jijini Dar es salaam mbele ya rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, mgeni rasmi Graca Machel, wakuu wa Balozi mbalimbali nchini na mashirika ya Umoja wa Mataifa.
Kutambuliwa kwake kuwa Balozi wa Kampeni ya Kupinga Ndoa za Utotoni, kutaleta hamasa zaidi na kumfanya kuongeza jitihada, nguvu na kutoa muda wake zaidi katika kutetea haki za watoto nchini Tanzania.
Valerie N. Msoka
Mkurugenzi Mtendaji
February 22,2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA kwa kushirikian na Shirika linalo hudumia Idadi ya Watu UNFPA Kinatoa mafunzo ya siku tatu kuhusiana na kuandika habari za uchunguzi wa unyanyasaji wa kijinsia.Mafunzo hayo yatatolewa kwa waandishi wa habari mapema tarehe 23 hadi Tarehe 25 Februari mwaka huu katika kanda tatu nchini Tanzania.
Mafunzo katika kanda ya Kaskazini yatajumuisha mikoa ya Arusha, Manyara Tanga na Kilimanjaro na yatafanyika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro. Katika Kanda ya Kati, waandishi wa habari watatoka mikoa ya Dodoma, Morogoro, Singida na Tabora ambapo mafunzo yatafanyika mjini Singida. Mafunzo katika Nyanda za Juu Kusini yatajumuisha mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe na Ruvuma na yatafanyika mjini Iringa.
Miongoni mwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na ubakaji,wanawake kurithiwa, watoto wa kike kulazimishwa kuolewa na ukeketaji kwa wawanamke na watoto.
Aidha TAMWA kupitia mradi yake imeweza Kujenga na Kuimarisha Usawa na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia kwa kutumia vyombo vya habari nchini. Imekuwa ikielimisha jamii namna ya kutambua ukatili wa kijinsia na madhara yake na kuitaka serikali na vyombo vya sheria kuweka mikakati itakayowezesha kuutokomeza.
TAMWA imesisitiza kuwa kama jamii na serikali hawatashirikiana kikamilifu kushughulikia vitendo vya ukatili wa kijinsia, itakuwa ni vigumu kutokomeza vitendo hivyo.
TAMWA inaamini kuwa endapo jamii itatoa taarifa mapema dhidi ya vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto pale vinapotokea, ingesaidia kuhakikisha vinashughulikiwa ipasavyo na hivyo kupungua kwa haraka na hatimaye kutokomezwa kabisa.
Valerie N. Msoka
Mkurugenzi Mtendaji
February 06,2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAMWA KUAZIMISHA SIKU YA UKEKETAJI MKOANI SINGIDA LEO
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 mwezi wa pili, 2015 saa 2:00 asubuhi kuadhimisha siku ya Kitaifa ya kupinga ukeketaji duniani ambayo mwaka huu kilele kitafanyika mkoani Singida.
Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Katala Beach Hotel (KBH) mjini Singida yanahusisha mikoa yote iliyoathirika na ukeketaji ili kuunganisha nguvu za wabunge, wakuu wa mikoa, polisi, mahakimu, viongozi wa dini, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya Umoja wa Mataifa, mashirkia ya kimaendeleo, wahanga wa vitendo hivyo, wanafunzi, walimu, wazee wa mila pamoja na ng’ariba ili kuweka mikakati ya kuondoa ukatili huo kutoka asilimia 15 hadi sifuri.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ni Mh. Sophia Simba huku kauli mbiu ikiwa ni “Piga vita ukeketaji” maadhimisho yanafanyika katika kipindi ambacho wanawake na wasichana zaidi ya 1,500 nchini hukeketwa kila msimu, hivyo yatajenga nguvu ya pamoja ili kuhakikisha vitendo hivyo vinapungua kama siyo kuisha kabisa.
TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapatiwa elimu ya kuondokana na mila kandamizi kwani zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake, kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia na taifa kwa ujumla.
Aidha TAMWA kwa ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa Linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), shirika ambalo limekuwa mstari wa mbele katika kutetea haki za watoto wa kike, imekuwa ikipinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto ukiwemo ukeketaji kwa kuelimisha jamii ili iondokane na mila hizo hasa katika mikoa ya Mara, Manyara, Dodoma, Singida, Arusha, Morogoro, Kilimanjaro na Tanga.
Valerie Msoka
Murugenzi Mtendaji
December 10, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTAFITI WA UNYANYASAJI KWA MAENDELEO YA MWANAMKE NA TAIFA
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini-TAMWA kikishirikiana na mashirika mengine manne ya kutetetea haki za wanawake na watoto , leo kinazindua ripoti ya utafiti kuhusu uelewa wa jamii juu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika ofisi zake za Sinza Mori, Dar es Salaam saa 3 asubuhi.
Ripoti ya Utafiti huo uliofanyika katika wilaya 10 zikiwemo 3 za visiwani ambazo ni (Pemba Kaskazini), Magharibi (Unguja Mjini Magharibi), Unguja Kusini na 7 za Tanzania Bara ambazo ni pamoja na Kisarawe (Pwani), Newala (Mtwara ), Mvomero (Morogoro), Lindi vijijini, Ruangwa (Mtwara), Kinondoni na Ilala, Dar es Salaam itatoa matokeo baada ya kumalizika kwa mradi huo unaojulikana kama (GEWE II)
Aidha kutokana na Utafiti mkubwa wa Hali ya Afya Tanzania (Demographic Health Survey) uliofanyika mwaka 2010 umeonyesha kuwa, vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 umeongezeka kutoka asilimia 33% miaka ya nyuma hadi kufikia asilimia asilimia 44% mwaka 2010.
TAMWA inaamini kuwa utafiti huu uliofadhiliwa na Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania utasaidia kuendelea kufichua hali halisi ya vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto vikiwemo, ukeketaji, ubakaji, vipigo kwa wanawake, mimba katika umri mdogo na vingine kama hivyo ambavyo vimekuwa vikimkwamisha mwanamke katika kuboresha maendeleo yake ya kijamii na kiuchumi.
TAMWA, katika utafiti huu imeshirikiana mashirika ya Mtandao wa Kijinsia Tanzania-TGNP, Chama cha Wanasheria Wanawake-TAWLA, Jumuiya ya WanawakeWanasheria Zanzibar (ZAFELA), na Kituo Cha Usuhishi-CRC ambayo pia yalishirikiana katika kutekeleza mradi huo.
Valerie N. Msoka
Mkurugenzi Mtendaji
PRESS RELEASE
GENDER BASED VIOLENCE SURVEY ON WOMEN AND NATIONAL DEVELOPMENT.
Tanzania Media Women Association (TAMWA) in collaboration with other four organizations that advocate for the rights of women and children, will today 10th December, 2014 launch a survey report on the community’s awareness of Gender Based Violence as perpetrated against children and women. The launch will take place at TAMWA’s office, Sinza Mori, Dar es Salaam.
The report was conducted in 10 districts among which include 3 in Zanzibar (Pemba North, Unguja West and Unguja South) and 7 from Mainland Tanzania namely Kisarawe (Cost), Newala (Mtwara ), Mvomero (Morogoro), Lindi Urban, Ruangwa (Mtwara), Kinondoni and Ilala (Dar es Salaam ). The findings of the study come following the completion of GEWE II Project.
In addition, according to the 2010 Demographic Health Survey, incidents of Gender Based Violence increased from 33% previously to 44% in 2010 among women of the age between 15 and 49. As a follow up on the existed situation and interventions made through GEWE II project which was therefore relevant and appropriate.
TAMWA believes that the Survey will contribute to the establishment of the context of Gender Based Violence against women and children in the country. The incidents of GBV in the society include Female Genital Mutilation (FGM), rape, beating, early pregnancy among others which hinder women social and economic development.
The survey was conducted by TAMWA in collaboration with other organizations including TGNP Mtandao, Tanzania Women Lawyers Association (TAWLA), Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA), Crisis Resolving Center (CRC) which have all been implementing GEWE II project which is supported by Danish Embassy in Tanzania.
Valerie N. Msoka
Executive Director
December 01,2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SIKU YA UKIMWI DUNIANI IADHIMISHWE KWA KUPINGA UKATILI KIJINSIA
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania-TAMWA kinaungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani ambayo hufanyika tarehe 1 Desemba kila mwaka, kikiitaka jamii kuvichukulia hatua vitendo vya unyanyasaji kijinsia ambavyo huchangia ongezeka la maambukizi ya Virusi Vinavyosababisha UKIMWI (VVU).
Miongoni mwa ukatili unaochangia ongezeko la VVU ni pamoja na ubakaji, wanawake kurithiwa, watoto wa kike kulazimishwa kuolewa na ukeketaji vitendo ambavyo hufanyika kwa wawanamke na watoto kwa kulazimishwa bila kujali hiari ya mtu husika.
Tafiti zinasema kuwa 5.1% ya Watanzania wenye umri kati ya miaka 15-49 wanaishi na VVU. Maambukizi ya VVU ni makubwa na kati ya hao wanawake ni 6.2% na wanaume ni 3.8% katika Tanzania Bara, kiwango cha maambukizi ya VVU ni miongoni mwa wanawake na wanaume wenye umri kati ya miaka 15-49 ambapo yamepungua kutoka 7.0% mwaka 2003-04 na 5.3% katika mwaka 2011-12.
TAMWA imesisitiza kuwa kama jamii na serikali havitashirikiana kikamilifu kushughulikia vitendo vya ukatili kijinsia kisheria, kauli mbiu ya mwaka huu ya “Tanzania Bila Maambukizi Mpya ya VVU, Vifo Vitokanavyo na UKIMWI na Ubaguzi na Unyanyapaa Inawezekana” haitaweza kufanikiwa.
Aidha TAMWA kupitia mradi wake wa Kujenga na Kuimarisha Usawa na Kutokomeza Ukatili wa Kijinsia (GEWE II) kwa kutumia vyombo vya habari nchini kimekuwa kikielimisha jamii namna ya kutambua ukatili wa kijinsia na madhara yake na kuitaka serikali na vyombo vya sheria kuweka mikakati itakayowezesha kuutokomeza.
TAMWA inaamini kuwa endapo jamii itavitolea taarifa mapema vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto pale vinapotokea na kuhakikisha vikavishughulikiwa ipasavyo, maambukizi ya UKIMWI yanaweza kupungua kwa haraka.
Valerie N. Msoka
Mkurugenzi Mtendaji
PRESS RELEASE
LETS COMMEMORATE WOLRD AIDS DAY WHILE FIGHTING GENDER BASED VIOLENCE
Tanzania Media Women Organization (TAMWA) joins Tanzanians to commemorate World AIDS Day which is annually commemorated on 1st December where as it calls on members of the community to take collective initiative against gender based violence acts which contribute to spread of HIV/AIDS.
Among the acts which contribute to spread of HIV include rape, inheriting women, forced marriage, Female Genital Mutilation among others. Most of people subjected to such acts are women, girls and children.
According to the third Tanzania HIV and Malaria Indicator Survey 2011 – 2012 (THMIS III), overall, 5.1% of Tanzanians age 15-49 are HIV-positive. HIV prevalence is higher among women (6.2%) than among men (3.8%). In Mainland Tanzania, HIV prevalence among women and men age 15-49 has decreased from 7.0% in the 2003-04 to 5.3% in the 2011-12.
TAMWA believes that if the government and people in the society are not cooperative to each other in the fight against GBV this year’s theme “Tanzania without new HIV infections, Deaths caused by HIV/AIDS, Discrimination and Stigma is possible” cannot be realized.
However, TAMWA’s Anti Gender Based Violence (GBV) programme of Building and Strengthening Gender Equality and Eradication of Violence against Women and Children (GEWE II) through the media has been providing education on the awareness of gender based violence acts and their effects calling on the government and legal organs to put in place strategies that would alleviate such acts.
TAMWA believes that if incidents of Gender Base Violence on women and children are timely reported and legal action taken against perpetrators spread of HIV will be equally reduced.
Valerie N. Msoka
Executive Director